Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kurejea nchini kwa staili hii
Habari za SiasaTangulizi

Lissu kurejea nchini kwa staili hii

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), atarejea nchini lakini hatokuwa peke yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kutokana na fikra za kushambuliwa na hata kuuawa zinazotawala kichwa chake, atarejea nchini akisindikizwa na ujumbe wa Kamati ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Lissu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, alishambiliwa kwa risasi jijini Dodoma tarehe 7 Septemba 2017, na kupelekwa nje kwa matibabu.

Kwenye ujumbe wake kwa watanzania alioutoa tarehe 4 Februari 2020, Lissu amesema, kamati hiyo imechukua uamuzi huo, baada ya kupokea malalamiko yake juu ya tukio la jaribio la kuuawa kwa risasi na kuvuliwa ubunge.

Ujumbe huo umeeleza, uongozi wa kamati hiyo uko katika mchakato wa kuwasilisha uamuzi huo kwa Bunge la Tanzania, ili kuomba ruhusa ya kutembelea Tanzania, kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa madai ya Lissu.

“Kamati inatambua kwamba ninataka kurudi Tanzania haraka iwezekanavyo, na inapendekeza kuwa ujumbe wa kamati inisindikize wakati nitakaporudi, kwa imani kwamba kutembelea Tanzania kutatoa fursa ya kukutana na mamlaka za kiserikali, kibunge na kimahakama, pamoja na wadau wengine, ili kuiwezesha Kamati kuelewa suala hili vizuri zaidi,” imeeleza taarifa ya Lissu. 

Ujumbe huo umeeleza zaidi kuwa, kamati hiyo imehoji vitisho vilivyotolewa dhidi ya Lissu.

“Kamati imesikitishwa na jaribio la mauaji dhidi yangu na tuhuma za kuhusika kwa mamlaka za kiserikali katika jaribio hilo. Mahsusi kabisa, kamati imehoji vitisho vilivyokuwa vinatolewa dhidi yangu kabla ya shambulio.

“Kuondolewa kwa walinzi wa eneo la makazi yangu muda mfupi kabla ya shambulio hilo, na kuondolewa na kupotezwa kwa kamera za CCTV kutoka kwenye jengo la makazi yangu. Kamati imeomba kupatiwa maelezo rasmi na ya kina kuhusu masuala haya, na taarifa rasmi kuhusu waliohusika na shambulio hilo.”

Wakati huo huo, Lissu ameshauri wabunge wapeleke malalamiko yao kwenye kamati ya IPU ili yachunguzwe.

“Ushauri wangu ni kwamba, wabunge wetu wote ambao wameathiriwa na vitendo hivi, wawasilishe malalamiko yao kwa IPU ili yachunguzwe.

“Kufanya hivyo kutaongeza shinikizo kwa utawala huu, pamoja na uongozi wa Bunge. Angalau wananchi wetu, Bunge na serikali watajua kwamba, vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu na za wabunge wa upinzani, zinamulikiwa taa ya dunia,” ameeleza Lissu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!