Lissu kupokelewa kifalme Dodoma

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati, kimeandaa mapokezi ya aina yake pindi Tundu Lissu atakapokanyaga ardhi ya jiji hilo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Lissu ambaye anatarajiwa kuchukua fomu ya urais katika Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kesho tarehe 8 Agosti 2020, anatajiwa kukutana na msururu wa watu watakaomsubiri barabarani baada ya kuchukua fomu hiyo.

Tayari wanasiasa mbalimbali waliopitishwa na vyama vyao kugombea urais, wamefika kwenye ofisi za tume hizo zilizopo eneo la Njedengwa kuchukua fomu akiwemo Dk. John Magufuli, mbombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa taarifa ya Gwamaka Mbughi, Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, wanachama wamejipanga kumpokea Lissu wakati akienda kuchukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wengine watasimama barabarani kumshangilia.

Amesema, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mgombea huyo kuingia Dodoma tangu atoke ughaibuni alikokuwa akipata matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jijini humo tarehe 7 Septemba 2017, akitokea bungeni eneo la Area D, atapokelewa kwa heshima ya chama na kuzungumza na wanachama pia.

“Mtakumbuka kwamba tarehe 4 Agosti 2020 Mkutano Mkuu wa Chadema Taifa ulimthibitisha Mh. Tundu Lissu kuwa mgombea wa nafasi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT).

“Siku ya tarehe 8 Agosti 2020 Mhe. Tundu Lissu atenda kuchukua fomu Ofisi za Tume ya Uchaguzi zilizopo Njendengwa mkoani Dododoma. Wanachama, viongozi na wadau wetu wote mnaalikwa kumsindikiza mgombea wetu katika ofisi hizo,” imeeleza taarifa hiyo.

Imefafanua kwamba, msafara utaanzia katika Ofisi za Kanda zilizopo  Area C Mtaa wa Makongoro kuanzia saa 3:00 Asubuhi na kwamba, utaratibu wa ziada utatolewa kwa kadri

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati, kimeandaa mapokezi ya aina yake pindi Tundu Lissu atakapokanyaga ardhi ya jiji hilo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea). Lissu ambaye anatarajiwa kuchukua fomu ya urais katika Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kesho tarehe 8 Agosti 2020, anatajiwa kukutana na msururu wa watu watakaomsubiri barabarani baada ya kuchukua fomu hiyo. Tayari wanasiasa mbalimbali waliopitishwa na vyama vyao kugombea urais, wamefika kwenye ofisi za tume hizo zilizopo eneo la Njedengwa kuchukua fomu akiwemo Dk. John Magufuli, mbombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa mujibu wa taarifa ya Gwamaka Mbughi, Katibu wa…

Review Overview

User Rating: 0.35 ( 1 votes)

About Danson Kaijage

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!