Lissu awawekea pingamizi Rais Magufuli, Prof. Lipumba 

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, amewawekea pingamizi wagombea wawili wa urais akidai wamekiuka Sheria za Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Waliowekewa pingamizi ni; Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Lissu amewasilisha pingamizi hilo leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020 ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma.

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, akiwasilisha fomu za pingamizi kwa wagombea wengine wa nafasi ya urais

Baada ya kutoka kuwasilisha mapingamizi hayo, Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema-Bara amesema “nimetoka ofisi za NEC kuwawekea mapingamizi wagombea John Pombe Magufuli wa CCM na Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF kwa kukiuka Sheria za Uchaguzi.”

O

“Hadi saa 10 na dk 5 hakukuwa na pingamizi lolote dhidi yangu. Saa ya mwisho ya mapingamizi ni saa 10 kamili,” ameandika.

John Magufuli, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, akirudisha fomu ya kuteuliwa nafasi hiyo kwa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage

Jana Jumanne, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliwateua wagombea 15 wa kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano yarehe 28 Oktoba 2020.

Pamoja na Lissu, wengine walioteuliwa ni; Rais John Pombe Magufuli (CCM), Leopard Mahona (NRA), John Shibuda (Ada Tadea), Mutamwega Mgaiwa (SAU), Cecilia Augustino Mwanga (Demokrasia Makini), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF.

Prof. Ibrahim Lipumba, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CUF, akirudisha fomu ya kuteuliwa nafasi hiyo kwa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage

Pia wamo, Philip John Fumbo (DP), Bernard Membe (ACT- Wazalendo), Qeen Cuthbert Sendiga (ADC), Twalib Ibrahim Kadege (UPDP), Hashimu Rungwe (Chaumma), Khalfan Mohamed Mazurui (UMD) na Seif Maalim Seif (AAFP).

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, amewawekea pingamizi wagombea wawili wa urais akidai wamekiuka Sheria za Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). Waliowekewa pingamizi ni; Rais John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama Cha Wananchi (CUF). Lissu amewasilisha pingamizi hilo leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020 ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma. …

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

3 comments

  1. Kama Lisu ameweka mapingamizi hayo kwa kufuata sheria na kanuni za uchaguzi na waliotuhumiwa ni chama cha ccm & cuf na kama wamekiuka bc haki itendeke watanzania tuwe wakweli na wenye kutenda haki

  2. Hana lolote huyo.anatafuta Kiki tu

  3. HIZO PINGAMIZI HAZINA MSHIKO HAPA TZ

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!