Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu atumia mtumbwi kuwafikia wapigakura
Habari za SiasaTangulizi

Lissu atumia mtumbwi kuwafikia wapigakura

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema akivuka Ziwa Victoria kwa kutumia kutumia mtumbwi akieleka Ukelewe
Spread the love

MSAFARA wa Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema umelazimika kutumia mtubwi kutoka Kisorya mkoani Mara kwenda Ukerewe Mkoa wa Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea)

Leo Jumatano tarehe 14 Oktoba 2020, msafara wa Lissu walifika eneo hilo la Kisorya ili kwenda Ukerewe umbali unaokadiliwa kuwa kilomita 21.9 kuhutubia mkutano wa kampeni lakini, kivuko kinachotoa huduma eneo hilo kilielezwa ni kibovu.

Kwa mujibu wa rariba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaonyesha mkutano wa kwanza Lissu anapaswa kuufanya Ukerewe kisha baadaye atakuwa Jimbo la Rorya Mkoa wa Mara.

 

Katika ukurasa wake wa Twitter, Lissu ameweka video wakiwa wanataka kuanza safari na kuandika “kwa mara ya pili katika kipindi hiki cha kampeni, bila sababu za msingi, hamna kivuko cha Kisorya kwa ajili ya msafara wetu kwenda Ukerewe.”

“Yote ni kwa ajili ya kuzuia tusifike huko. Sasa tutavuka kivingine na tutafanya mkutano kama ilivyo ratiba! Haturudi nyuma,” amesema Lissu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!