Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu atua Tanzania, shangwe zatawala
Habari za SiasaTangulizi

Lissu atua Tanzania, shangwe zatawala

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema (katikati) akiwasili uwanja Ndege JK Nyerere. Kushoto Freeman Mbowe na John Mnyika (kulia).
Spread the love

TUNDU Antiphas Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania cha Chadema- Bara amewasilia nchii hum oleo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu amewasilia nchini Tanzania akitokea Ubelgiji kwa ndege ya Shairika la Ethiopia na kupokelewa na viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Baada ya kuwasilia, umati ya watu waliojitokeza kumpokea mwanasiasa huyo, umeanza msafara kutoka uwanjani hapo kwenda Ofisi za Makamu Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kutoka ndani akiwa ameongozana na viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho na Katibu Mkuu wake, John Mnyika, shangwe zilitawala uwanjani hapo.

Sauti za nyimbo zilisikika zikiimba ‘Rais, Rais, Rais, Rais’ hali iliyowafanya walinzi kutumia nguvu kuwaweka kando.

Kila mmoja alitaka kumsogelea amguse Lissu.

Lissu amerejea nchini mwake ikiwa imepita miaka takribani mitatu tangu alipokuwa nje ya nchi kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwa risasi zaidi ya 30.

Tukio hilo lilitokea mchana wa tarehe 7 Septemba 2017 katika makazi yake Area D jijini Dodoma na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa matibabu.

Usiku huohuo alisafirishwa akiwa hajitambui kwenda Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi hadi tarehe 6 Januari 2018 alipohamishwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!