TUNDU Lissu, Mbunge was Singida Mashariki amesema kuwa upinzani umeshambuliwa kuliko kipindi chochote nchini Tanzania. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).
Lissu amesema hivyo leo tarehe 28 Agosti 2018 usiku saa 3:23 alipozungumza katika kipindi cha BBC Swahili.
Mbunge huyo aliyepigwa risasi mjini Dodoma yapata mwaka mmoja uliopita amesema katika kipindi cha miaka miwili ya sasa, upinzani umeshambuliwa kwa kiwango kikubwa.
Alisema hivyo baada ya kuulizwa swali na mtangazaji Zuhura Yunus kwamba, upinzani umelegalega nchini Tanzania.
Alijibu swali hilo Lissu amesema, itakua ajabu kama upinzani utabaki vile katika kipindi hiki.
“Wapinzania hawajanyamaza, ila umeshambuliwa,” amesema Lissu na kuongeza “ni ajabu kama tungeendelea kuwa kama wa Kikwete (Rais Kikwete, Rais Mkapa).
Pia Lissu amesema kuwa, Bunge lilitoa taarifa ya kukataa kumlipia matibabu kwa madai ya kutofuata utaratibu.
Amesema, atapona vizuri atarejea nchini huku akiwa na tahadhari.
Leave a comment