Lissu atikiswa, chopa yake yagomewa

Spread the love

HELKOPTA (chopa) iliyotarajiwa kumbeba Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani, imegomewa kuruka. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka Chadema zinaeleza, Lissu na timu yake ya kampeni, walikuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Malimu Julius Nyerere (JNIA), tayari kuingia kwenye chopa hiyo na kuanza safari ya kuelekea Bagamoyo ili kuendelea na kampeni.

Ratiba ya mikutano mitano ya kampeni za Lissu ilionesha kwamba, Lissu angekuwa na mkutano wa hadhara leo tarehe 10 Septemba 2020 Bagamoyo.

Taarifa ya Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho imeeleza, kwamba Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA), ndio iliyotoa barua ya kuzuia chopa hiyo kuruka. hata hivyo, hakueleza sababu zilizotolewa na TCAA.

“Taarifa za kukataliwa kwa helikopta hiyo kuruka, zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa wakati msafara wa Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama uwanjani,” imeeleza taarifa ya Makene.

Makene amesema, kutokana na katazo la TCAA, chama hicho kimelazimika kutafuta utaratibu mwingine wa kuweza kufanikisha safari ya Lissu kwenda kwenye mkutano huo. 

HELKOPTA (chopa) iliyotarajiwa kumbeba Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani, imegomewa kuruka. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea). Taarifa kutoka Chadema zinaeleza, Lissu na timu yake ya kampeni, walikuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Malimu Julius Nyerere (JNIA), tayari kuingia kwenye chopa hiyo na kuanza safari ya kuelekea Bagamoyo ili kuendelea na kampeni. Ratiba ya mikutano mitano ya kampeni za Lissu ilionesha kwamba, Lissu angekuwa na mkutano wa hadhara leo tarehe 10 Septemba 2020 Bagamoyo. Taarifa ya Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya…

Review Overview

User Rating: 4.1 ( 1 votes)

About Regina Mkonde

One comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!