Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu apigilia msumali wabunge viti maalum Chadema
Habari za Siasa

Lissu apigilia msumali wabunge viti maalum Chadema

Spread the love

TUNDU Lissu, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameendelea kupinga chama hicho kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaan … (endelea). 

Lissu ni miongoni mwa viongozi wa Chadema, wanaopinga suala hilo kwa madai, kufanya hivyo ni sawa na kuwasaliti wananchi waliowapigia kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Katika uchaguzi huo, chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuibuka na ushindi mkubwa wa madiwani, wabunge na urais ambao haujawahi kutokea tangu mwaka 1995 ulipoanza uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

Hata hivyo, Chadema na ACT-Wazalendo ni miongoni mwa vyama vya siasa, vilivyopinga matokeo hayo kwa madai, uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu.

Kutokana na hali hiyo, Chadema ambacho kwa mujibu wa sheria, kimejipatia viti 19 vya wabunge wa viti maalum, kumekuwa na mjadala mzito ndani na nje ya chama hicho kuhusu je, wapeleke majina NEC ili yateuliwe au wasifanye hivyo kwani wamekwisha kusema haukuwa uchaguzi halali?

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema (Bara), amekuwa akipinga waziwazi chama hicho kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni au madiwani akisema “haukuwa uchaguzi, ulikuwa uchaguzi.”

Mwansiasa huyo aliyeondoka juzi Jumanne tarehe 10 Novemba 2020 kwenda nchini Ubelgiji kwa kile alichodai “kuendelea kubaki Tanzania, maisha yangu yangekuwa hatarini” ametoa waraka wa kusisitiza chama hicho kutokubali kuteua majina ya viti maalum.

Lissu ametoa waraka huo kipindi ambacho, taarifa za ndani ya chama hicho zinaeleza, Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), limekuwa likishinikiza kupelekwa kwa majina hayo NEC.

Halima Mdee

Waraka huo wa Lissu, kama ulivyo huu hapa chini;

Hiki chama hakijarudishwa mwaka ‘95. Chama hiki leo ni kikubwa kuliko chama kingine chochote cha siasa Tanzania (CCM sio chama cha siasa, ni chama-dola).

Chama hiki leo kina wanachama zaidi ya milioni sita walioandikishwa; na uongozi uliochaguliwa katika kila ngazi ya uongozi nchi nzima.

Chama hiki kimedhihirisha kwamba kinaungwa mkono na mamilioni ya Watanzania wa makundi yote na rika zote. Ushahidi ni kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Chama hiki kimedhihirisha pia kwamba bila matumizi ya nguvu za kijeshi za dola chama hiki hakiwezi kushindwa uchaguzi wowote katika nchi hii.

Hakukuwa na chama cha aina hii mwaka ‘95 au katika kipindi kingine chochote cha historia yetu. Sasa kipo, labda mtu asiwe na macho ya kuona au akili ya kutambua.

Kufikiria kwamba chama ni wabunge au madiwani tu ni kukosa kuelewa maana ya chama cha siasa katika mazingira halisi ya nchi yetu.

Tundu Lissu, aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema akiwasili nchini Ubelgiji

Ni kuangalia mambo kwa macho ya maslahi yetu binafsi na kushindwa kuangalia kwa miwani ya maslahi mapana ya wananchi wetu. Na hilo ndio tatizo la baadhi yetu!!!

Kibaya tunachotakiwa kukiepuka ni kuruhusu watu wenye vijimaslahi vyao kukiharibu chama kwa kutuaminisha kwamba bila wao kuwa wabunge au madiwani basi hakuna chama.

Tunachopigania sio nani wawe wabunge au madiwani tu. Kama hiyo ndio ingekuwa lengo letu tungeshapeleka majina ya wabunge na madiwani wa Viti Maalum wote.

Tunachopigania ni wananchi wetu wawe na Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu. Lengo hilo linahitaji tuwe na wabunge na madiwani waliopatikana kwa njia halali, sio wa kupewa zawadi na walioharibu Uchaguzi Mkuu.

Kuwa na wabunge na madiwani katika mazingira ambayo yatahalalisha utawala huu haramu ndio kutakakoumiza na kuharibu chama chetu kuliko kitu kingine chochote.

Ndio maana maCCM na wapambe wao wanataka sana tupeleke wabunge wa Viti Maalum bungeni. Wanajua hilo ndio litakuwa tambara la kudekia na kuhalalisha uharamu wa uchafuzi wao. Na ndio njia itakayoumiza chama chetu kuliko magereza yote ya Magufuli.

6 Comments

  • Bwana Mbowe mwenyekiti wangu chama cha siasa siyo wabunge wala madiwani bali ni wanachama wenye uchungu na chama chao kama ni kukiimarisha chama kifedha rudi kwa wanachama. TANU kiliendeshwa na kuimarishwa kwa michango ya wanachama na siyo ruzuku haramu ya wakoloni.ANC kiliendeshwa na kuimarishwa na wanachama wazalendo.CCM ni chama dola au chamakoloni kimuundo na kiutendaji. Watatumia viti maalumu kuwakejeli na kuwadhalilisha. Hamkushindwa kwenye mapambano wamewapora. MBOWE ACHANA NA WAROHO WA FEDHA. CHADEMA KIKO HAI NA KITAKUWA HAI 2025. KITAKUWA NA NGUVU YA AJABU.

  • Mkisusa wenzenu wala. Najua hoja ya Lissu imewakamata wengi huko akiwemo Mwenyekiti wenu wa ruzuku. Kama hamuitaki hiyo ruzuku, tutaona uhai wa Chadomo miaka miwili hii. Na wala huo sio mtego, bali haki ya kikanuni na kimahesabu kwa wamama wote wa nchi hii. Kama hamuitaki, basi bhaana. Tusiwalazimishe.

  • Chama kitapasukia hapa, who has the final say, mwenyekiti ambaye hajakimbia wanachama wake au makamu mwenyekiti aliyepo ughaibuni?

  • Chadema ni Chama makini kupita maelezo. Sina shaka na maamuzi haya ya viongozi kwani yana mantiki na tija si kwa chama tu bali kwa Taifa zima.Ukitaka kupoteza uhuru wako na haki basi endekeza shida ya Tumbo, hilo CDM tunalijua na hakuna mtego wa tumbo utatunasa. Chadema iko ndani ya mioyo ya Watanzania na si kwenye tumbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!