Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu amwomba Rais Magufuli ajiandae kumpokea
Habari za Siasa

Lissu amwomba Rais Magufuli ajiandae kumpokea

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amemshauri Rais Magufuli kufanya maandalizi ya kumkabidhi nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Makamu huyo mwenyekiti wa Chadema, kwa zaidi ya miaka miwili anaishi nje ya Tanzania, alikokwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D jijini Dodoma tarehe 7 Septemba 2017.

Leo Jumanne tarehe 9 Juni 2020, Lissu amesema Rais Magufuli atapewa ratiba rasmi ya ujio wake, pindi wakati utakapofika, huku akisisitiza atakuwa mgeni wa kiongozi huyo wa Tanzania.

“Nitarejea Tanzania na nitakuwa mgeni wa Rais Magufuli, na mheshimiwa Rais Magufuli ataambiwa nitarejea muda gani na tarehe gani na dunia ikiwa inaniangalia,” amesema Lissu.

Lissu ametoa salamu hizo, wakati akizungumzia tukio la kushambuliwa kwa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo akiwa katika makazi yake Area D Dodoma.

Lissu ambaye pia ni mhanga wa tukio la kushambuliwa na watu wasiojulikana, amesema hana imani kama vyombo vya ulinzi na usalama vitalifanyia kazi suala hilo, ikiwemo kufanya uchunguzi kwa ajili ya kubaini wahusika na kuwachukulia hatua.

Amedai kuwa, hana imani juu ya suala hilo kwa kuwa, vyombo hivyo mpaka sasa havijafanyia kazi tukio la kushambuliwa kwake na watu wasiojulikana.

Hata hivyo, mara kadhaa Jeshi la Polisi limenukuliwa na vyombo vya habari likimtuhumu Lissu kwamba anakwamisha uchunguzi wa tukio hilo, kutokana na kushindwa kuitikia wito wake wa kurudi nchini kwa ajili ya mahojiano.

Lissu amedai, mwendelezo wa matukio ya viongozi wa upinzani kushambuliwa na watu wasiojulikana, lengo lake ni kuwafanya Watanzania wasiendelee na harakati za kudai demokrasia nchini.

Amesema matukio ya wapinzani kushambuliwa yanasababishwa na maadui wa kisiasa wa Chadema, kwa kuwa ndani ya chama hicho hakuna mvutano wa aina yoyote.

“Ndani ya Chadema hakuna mvutano wa aina yoyote, wale wa kutumwa wameshaondoka. Chama kiko kwenye utulivu, haya ni matendo ya m aadui zetu w a kisiasa,” amesema Lissu.

Tangu taarifa za tukio la kushambuliwa kwa Mbowe zisambae, kumeibuka mijadala ambapo baadhi ya watu wanadai limelenga kuzima hotuba ya Lissu aliyoitoa jana, kuhusu nia yake ya kugombea Urais wa Tanzania, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, kupitia Chadema.

Akizungumzia madai hayo, Lissu amesema tukio la Mbowe haliwezi kuzima mjadala wa uchaguzi, bali linaongeza joto la uchaguzi huo.

“Haya matukio yana uhusiano, wanafikiri wanahamisha mjadala wa uchaguzi. Badala ya kuhamisha mjadala wa uchaguzi wataukuza zaidi, sababu matukio ya namna hii hayanyamazishi watu bali yanaongeza kelele, kama wanafikiri watu watasahau kwa shambulio la Mbowe, wanakosea,” amesema Lissu.

Lissu amesema tukio la kushambuliwa kwa Mbowe limeifanya Chadema kuwa imara zaidi ilivyokuwa hapo awali.

“Tuko vizuri tuna chama kikubwa,  imara na tuna mizizi mirefu kuliko ilivyokuwa mwaka 2017. Ili shambulio la sasa linatukamoza tutasimama tu,” amesema Lissu.

Mapema leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Gilles Muroto amepiga marufuku mtu au kikundi cha watu kutumia tukio la Mbowe kwa mtaji wa kisiasa na kutaka polisi waachwe wafanye uchunguzi na utakapokamilika watatoa taarifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!