June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lissu ‘ampasua’ Spika Ndugai

Spread the love

TUNDU Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki amemshangaa Spika Job Ndugai, kwa madai ya kufanya kazi kama ‘mkusanya mapato ya benki.’Anaripoti Mwandishi wetu… (endelea)

Amesema, anachokitaka kwa Bunge kipo kwa mijubu wa sheria na sio ‘hongo’ ambayo hutolewa gizani.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo tarehe 7 Aprili 2020, Lissu amabye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Spika Ndugai, kudai mbunge huyo halidai Bunge.

Spika Ndugai jana tarehe 6 Aprili 2020, alisema Lissu ameshalipwa posho zake zote, na hakuna anachodai. Lissu amesema, stahili zake anazohitaji ni pamoja na gharama za matibabu pamoja na kiinua mgongo cha wakati akitumikia Bunge.

“Zote hizo ambazo hazijalipwa, zipo kwa mujibu wa sheria. Badala ya kuzungumzia hizo ambazo ndio nilisema ninazidai, analeta habari za madeni yangu ya benki.

“Tangu lini Spika wa Bunge la Tanzania amekuwa mkusanya madeni kwa niaba ya benki za biashara?”amehoji Lissu na kuongeza “sijalalamika kutolipwa mshahara wa Bunge, bali madai gharama za matibabu.”

Amehoji, kwanini Spika Ndugai anaishia kuzungumzia malipo ya posho na mishahara pekee? pasina kugusia masuala ya matibabu yake na kiinua mgongo.

Akiwa bungeni, Spika Ndugai alimkumbusha Lissu kuhusu mikopo yake aliyochukua sehemu mbalimbali yenye thamani zaidi ya Sh. 70 milioni, akimtaka alipe.

“Lissu anapenda sana mambo yake kujadiliwa kwenye public (wazi), mimi nilishakataa kabisa sipendi, huwa nasema kwa sababu nakuwa nimechokozwa na jambo Fulani.

“Nataka kuwathibitishia kwamba posho zake zote amelipwa, mpaka hiyo ya Juni 2019 amelipwa,” alisema Spika Ndugai.

Hata hivyo Lissu amesema “haki zangu ni pamoja na kiinua mgongo (gratuity) ambayo ni 40% ya mishahara yote ya kipindi nilichotumikia. Je, umemsikia akisema hiyo imelipwa?

“Madai yangu ni pamoja na gharama za matibabu na za kujikimu wakati wote nikiwa kwenye matibabu. Umemsikia akisema na hiyo imelipwa?” amehoji Lissu.

error: Content is protected !!