Tundu Lissu, mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Lissu akumbana na kikwazo Chato

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekumbana na kituko cha kwanza Chato mkoani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Taarifa kutoka Chato zinaeleza, usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe 13 Oktoba 2020, eneo la biashara la Masai  Machae, mgombea ubunge kupitia chama hicho katika jimbo hilo, limevamiwa na kuvunjwa.

Lissu kwenye ukurasa wake wa twitter amesema, licha ya uvamizi na vitisho hivyo, mkutano wake wa kampeni aliopanga kuufanya leo, utatekelezwa bila hofu yoyote.

“Leo ni siku ya mkutano wetu Jimbo la Chato na tayari wameanza kutufanyia fujo. Usiku wa kuamkia leo wamevamia biashara ya Mgombea ubunge wetu na nyumba ya Katibu wa Jimbo na kuharibu mali zao. Hatutishiki na hatutatishika. Mkutano wetu wa Chato uko pale pale,” amesema Lissu.

Mgombea huyo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chadema, anamalizia kampeni zake katika Mkoa wa Shinyanga na leo atafanya kampeni majimbo ya Bukombe, Mbogwe na mkutano wa mwisho utakuwa Chato.

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekumbana na kituko cha kwanza Chato mkoani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea). Taarifa kutoka Chato zinaeleza, usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe 13 Oktoba 2020, eneo la biashara la Masai  Machae, mgombea ubunge kupitia chama hicho katika jimbo hilo, limevamiwa na kuvunjwa. Lissu kwenye ukurasa wake wa twitter amesema, licha ya uvamizi na vitisho hivyo, mkutano wake wa kampeni aliopanga kuufanya leo, utatekelezwa bila hofu yoyote. “Leo ni siku ya mkutano wetu Jimbo la Chato na tayari wameanza kutufanyia fujo. Usiku wa kuamkia leo wamevamia…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!