Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aitisha maombi ya kitaifa
Habari za Siasa

Lissu aitisha maombi ya kitaifa

Spread the love

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu ametoa wito kwa Watanzania wa dini zote kufanya maombi ya kitaifa Jumatatu ya tarehe 26 Oktoba 2020, ili kumuomba Mungu alivushe salama Taifa hilo katika Uchaguzi Mkuu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Lissu ametoa ombi hilo leo Ijumaa tarehe 23 Oktoba 2020 kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mgombea huyo wa Urais wa Chadema amewaomba Watanzania popote walipo waitumie siku hiyo kufanya maombi, dua na sala ili uchaguzi huo utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 uwe huru na wa haki.

“Watanzania wenzangu, hii ni wiki ya mwisho ya uchaguzi mkuu muhimu kuliko mwengine yoyote katika historia yetu, Jumatano ijayo mtaenda kupiga kura kuchagua viongozi. “

“Katika kipindi muhimu kama hiki, nawaomba Watanzania wenzangu wote, wa dini zote, tushirikiane kuiombea nchi yetu tuwe na uchaguzi huru, haki na unaokubalika na Watanzania wote na unaoeleweka na dunia yote ambayo sisi ni sehemu yake,” amesema Lissu.

Uchaguzi huo utahusisha wa madiwani, wabunge, wawakilishi upamnde wa Zanzibar pamoja na Marais wa Tanzania na Zanzibar

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!