Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu ‘afukua makaburi’ Mbarali
Habari za Siasa

Lissu ‘afukua makaburi’ Mbarali

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, ugomvi wa wakulima na wafugaji ‘ni la kuundwa.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbarali … (endelea).

Kwenye mkutano wake wa kampeni za rais Mbarali, Lissu amesema, maeneo yenye migogoro awali yalikuwa ni mashamba ya wananchi, kisha yakachukuliwa na serikali na baadaye yakakabidhiwa wawekezaji ambao nao badala ya kulima, wanayakodisha.

“Ukienda Mkoa wa Morogoro Wilaya ya Mvomero, Kilosa na Kilombero, hizo wilaya tatu za Morogoro ndio kitovu cha migogoro ya wakulima na wafugaji. Sasa imehamia Mbarali mkoa wa Mbeya.”

“Ukiemda Bonde la Rufiji sasa kuna migogoro ya wakulima na wafugaji, ukienda Rukwa kwenye Hifadhi ya Katavi sasa kuna migogoro ya wakulima na wafugaji.”

“Kitu gani kinafanyika? kitu gani kinaendelea nchi hii? kwani wafugaji wameanza kufuga jana? watu wameanza kulima juzi? hawa watu walikuwa wanapigana miaka yote? kwanini sasa wanapigana? mnafahamu kitu gani kinaendelea?” amehoji Lissu.

Akieleza kiini cha matatizo ya ardhi Mbarali, Lissu alianza kwa kuwafikirisha wananchi kwamba, nani anamiliki ardhi kubwa?

“Nani anayemiliki sehemu kubwa ya ardhi ya Mbarali! haya mashamba ya mpunga. Haya si yalikuwa mashamba ya NAFCO? wamewapa watu binafsi, wameyatumia yote? wanakodisha sio?

“Sasa yalikuwa mashamba ya serikali yaliyochukuliwa kutoka kwa wananchi, halafu serikali ilipoacha kuyalima badala ya kuwarudishia wananchi, ikawapa watu wanaoitwa wawekezaji. Matokeo yake wananchi wana shida ya ardhi, maeneo yaliyokuwa ya wafugaji yamefanywa kuwa hifadhi ya taifa, wafugaji wamefukuzwa.”

Amesema, matatizo na msingi wa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wagaji inafafana akitolea mifano sehemu zenye hifadhi ikiwemo Arusha.

“Ukienda Morogoro ni hivyo hivyo, ukienda Arusha ni hivyo hivyo. Mahali penye hifadhi, watu wamefukuzwa. “Huku mnanyang’anywa mashamba, kule wafugaji wamefukuzwa wanataka ardhi ya kufuga, nyinyi mnatafuta mashamba, adhi imekuwa ndogo ugovi utaacha kutokea?” amehoji.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!