Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu achukua fomu urais Tanzania, asindikizwa kwa msafara NEC
Habari za SiasaTangulizi

Lissu achukua fomu urais Tanzania, asindikizwa kwa msafara NEC

Tundu Lissu-Chadema
Spread the love

TUNDU Antiphas Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema amekabidhiwa fomu za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020 na Tume ya Taifa (NEC) jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Lissu na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu amekabidhiwa fomu hizo leo Jumamosi tarehe 8 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu, Semistocles Kaijage.

Kabla ya kukabidhi fomu hizo, Jaji Kaijage amesema, siku ya uteuzi ni tarehe 25 Agosti 2020 na siku hiyo wagombea watakuwa na fursa ya kuwasilisha fomu hizo.

“Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na sharia ya uchaguzi, ikishajiridhisha mnayo sifa mtateuliwa,” amesema Jaji Kaijage huku akiwapongeza wagombea hao kwa kujitokeza kuwania nafasi hiyo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Charles Mahera kuna suala la kutafuta wadhamini katika mikoa 10 kati ya hizo, mikoa miwili iwe ya Zanzibar na kila mkoa mmoja angalau uwe na wadhamini 200.

Dk. Mahera amesema, wametoa fursa kwa madhumuni ya kuja kukagua fomu kama mtambenda siku tatu kabla ya uteuzi kuanzia tarehe 22 hadi 24 Agosti 2020 ili kukwepa mambo yanayoweza kujitokeza siku ya uteuzi 25 Agosti 2020.

 

Kabla ya kufika ofisi za NEC, Lissu na Mwalimu walianzia ofisi za Chadema Kanda ya Kati ambapo walisaini kitambu cha wageni ambapo kulikuwa na viongozi mbalimbali na wanachama wa chama hicho.

Mara baada ya kumaliza, msafara uliondoka ofisini hapo mida ya saa 4:30 asubuhi ukisindikiza na bodaboda, bajeji na magari ukafika ofisi za tume saa 4:55 asubuhi.

Ulipokuwa ukipita msafara huo, watu mbalimbali walisimama kuushuhudia na kusimamisha baadhi ya shughuli kwa wananchi wa Jiji hilo.

Mara baada ya kumaliza kukabidhiwa fomu hizo, msafara huo ulirejea tena ofisini hizo za Kanda.

Baadhi ya viongozi waliomsindikiza ni wabunge wanaiomaliza muda wake, Godbless Lema (Arusha Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Susan Kiwanga (Mlimba) wenyeviti wa kada na wanachama.

 

Ni magari mawili tu yaliyoruhusiwa kuingia ndani ya ofisi hizo lile lililombeba Lissu na mgombea wake mwenza, Mwalimu huku mengine yakibaki nje.

Pia, walioingia kukabidhiwa fomu hizo ni wachache na wengine wakatakiwa kubaki nje wakisubiri kukamilika shughuli hiyo.

Vyama vilivyokwisha kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ni; AAFP, NRA, DP, CCM, SAU, ADC, UPDP, Demokrasia Makini na ACT- Wazalendo.

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu ulianza tarehe 5 -25 Agosti 2020 na kampeni zitaanza 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020 na siku inayofuata ya Jumatano utafanyika Uchaguzi Mkuu huo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!