Wachezaji wa Simba na Yanga wakiingia uwanjani

Ligi Kuu Bara kurejea Juni 13, 2020

Spread the love

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo ametangaza tarehe ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo ni Juni 13, huku ratiba kamili ikitarajiwa kupangwa Mei 31, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kuendelea kwa michezo hiyo ni kufuatia agizo la Rais John Magufuli kutanga shughuli za michezo kuendelea kufuatia kuwepo kwa mwenendo mzuri wa mlipuko wa ugonjwa Corona nchini.

Taarifa ya kuendelea na michezo hiyo kutoka bodi ya Ligi imetolewa kwenye kurasa yao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kuwa na vikao vya muda mrefu na kusubiri muongozo kutoka Serikalini.

Baada ya agizo hilo baadhi ya klabu mbalimbali wa Ligi Kuu tayari zimeanza maandalizi ya kumalizia michezo iliyosalia ambayo itachezwa katika kituo kimoja Jijini Dae es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Uhuru na Azam Complex.

Ligi hiyo ilisimama mwezi Machi kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya kutaka shughuli zote za michezo kusimama kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19, huku klabu ya Simba ikiwa vinara kwenye msimamo wakiwa na alama 72.

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo ametangaza tarehe ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo ni Juni 13, huku ratiba kamili ikitarajiwa kupangwa Mei 31, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam ... (endelea). Kuendelea kwa michezo hiyo ni kufuatia agizo la Rais John Magufuli kutanga shughuli za michezo kuendelea kufuatia kuwepo kwa mwenendo mzuri wa mlipuko wa ugonjwa Corona nchini. Taarifa ya kuendelea na michezo hiyo kutoka bodi ya Ligi imetolewa kwenye kurasa yao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kuwa na vikao vya muda mrefu na kusubiri muongozo kutoka Serikalini. Baada…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!