Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lema: Hata mkiniletea CCM wote Arusha, nitashinda
Habari za Siasa

Lema: Hata mkiniletea CCM wote Arusha, nitashinda

Godbless Lema, Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema)
Spread the love

GODBLESS Lema, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini na Mbunge wa Arusha Mjini anayemaliza muda wake, amesema sheria ingeruhusu, angetaka wagombea wote wa CCM Arusha ashindane nao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Lema amechukua fomu ya kugombea jimbo hilo kwa awamu ya tatu, kwenye ofisi ya Kanda ya Kaskazini tarehe 10 Julai 2020. Ameanza kuwa mbunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

“Nimesikia sikia majina ya wagombea Ubunge Arusha Mjini kupitia CCM. Kama sheria ingeruhusu, wote 30 kushindana nami na picha zao wote kutokea kwenye karatasi ya kura dhidi yangu, bado wangeimba wimbo walioimba 2010/2015. Twendeni mpaka mwanzo wa bahari, wepesi sana hawa,” ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa twitter.

Hata hivyo, kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020, Lema amewaambia wakazi wa Arusha hususani Jimbo la Arusha Mjini kwamba, watashinda.

“Tuna washinda tena. Msiogope,” Lema amewatia moyo wapigakura na wapenzi wa Chadema jijini humo.

Leo, CCM imefungua pazia kwa wanachama wake kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo, zoezi hilo linatarajiwa kusitishwa tarehe 17 Julai 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!