Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini

Lema asakwa Dar

Spread the love

JESHI la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadaiwa kuzingira Hoteli ya Regency Park iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam likimsaka Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Lema kupitia ukurasa wake wa twitter leo tarehe 17 Machi 2020, ameandika kwamba, polisi kadhaa waliovaa kiraia wamezingira hoteli hiyo.

“Polisi wengi wakiwa na magari wamevamia Hotel ninayo fikia Regency Park Mikocheni, nimepata taarifa kuwa wananitafuta,” ameandika Lema.

Chadema katika ukurasa wake wa twitter kimeeleza kwamba, hadi sasa hakijafahamu sababu za mbunge wake kusakwa na polisi.

Na kwamba, Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alipanga kufanya mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, kujibu kauli ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, DPP Biswalo Mganga, kwamba atamfungulia kesi kutokana na kutoa taarifa za uongoz juu ya Jeshi la Polisi mkoani Singida.

JESHI la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadaiwa kuzingira Hoteli ya Regency Park iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam likimsaka Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam ... (endelea). Lema kupitia ukurasa wake wa twitter leo tarehe 17 Machi 2020, ameandika kwamba, polisi kadhaa waliovaa kiraia wamezingira hoteli hiyo. "Polisi wengi wakiwa na magari wamevamia Hotel ninayo fikia Regency Park Mikocheni, nimepata taarifa kuwa wananitafuta," ameandika Lema. Chadema katika ukurasa wake wa twitter kimeeleza kwamba, hadi sasa hakijafahamu sababu za mbunge wake kusakwa na polisi. https://twitter.com/godbless_lema/status/1239793753604395009 Na kwamba, Lema ambaye ni Waziri…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!