Godwin Kunambi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma

LAPF ‘yapiga tafu’ Dodoma

MFUKO wa Pensheni wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) umekabidhi hundi ya Sh. 6 milioni kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kutatua tatizo la uhaba wa maji katika maeneo ya Ihumwa na Mtumba mkoani humo, anaandika Dany Tibason.

Leo akikabidhi hundi hiyo kwa Godwin Kunambi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma mjini humo, James Mlowe ambaye ni Meneja Mawasiliano na Masoko wa LAPF amesema, mfuko huo umetoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufufua visima vya maji vilivyoharibika.

Amesema mfuko huo ulipokea maombi kutoka katika Ofisi ya Manispaa pamoja na ofisi ya mbunge kupatiwa msaada wa kutengeneza visima vya maji katika Kata ya Ihumwa na Mtumba kutokana na visima hivyo kuharibika na kuwasababishia usumbufu wa kukosea maji wakazi hao.

Amesema LAPF kama taasisi ya serikali, imekuwa ikifanya shughuli nyingi na halmashauri mbalimbali nchini hususani shughuli za maendeleo.

“Kwa sasa Dodoma ni Makao Mkuu ya Nchi hivyo kuna watu wengi watahamia hivyo hakuna sababu ya kuwepo ukosefu wa maji.

“Kadri watu wanavyoongezeka ndivyo mahitaji yanavyoongezeka hivyo mahitaji ya maji ni makubwa zaidi katika Mji wa Dodoma na Ihumwa na Mtumba ni sehemu mahitaji hayo,” amesema Mlowe.

Hata hivyo Mlowe amesema, pesa zinazotolewa na taasisi mbalimbali pamoja na wahisani ni vyema zikatumiwa kwa majengo yaliyokusudiwa badala ya kuzibadilishia matumizi.

Hata hivyo, Kunambi amesema katika uongozi wake, atahakikisha miradi yote iliyokusudiwa inafanyika.

“Ni kweli kwa sasa Dodoma kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa maji katika maeneo ambayo yapo nje ya mji.

“Msaada ambao tumeupata kutoka LAPF utasaidia kuboresha na kukarabati visima vya maji ili wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa maji,”amesema Kunambi.

MFUKO wa Pensheni wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) umekabidhi hundi ya Sh. 6 milioni kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kutatua tatizo la uhaba wa maji katika maeneo ya Ihumwa na Mtumba mkoani humo, anaandika Dany Tibason. Leo akikabidhi hundi hiyo kwa Godwin Kunambi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma mjini humo, James Mlowe ambaye ni Meneja Mawasiliano na Masoko wa LAPF amesema, mfuko huo umetoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufufua visima vya maji vilivyoharibika. Amesema mfuko huo ulipokea maombi kutoka katika Ofisi ya Manispaa pamoja na ofisi ya mbunge kupatiwa msaada wa kutengeneza visima…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube