Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kwa nini tunaumba Miungu itakayogharimu taifa?
Habari za Siasa

Kwa nini tunaumba Miungu itakayogharimu taifa?

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi
Spread the love

SERIKALI iko mbioni kuwasilisha bungeni muswada wa Sheria ya Utekelezaji wa Haki na wajibu wa Msingi, Sura ya 3 (The Basic Rights and Duties Enforcement Act Cap 3). Muswada huu, unaingia bungeni kupitia “muswada wa mabadiriko ya sheria mbali mbali.” Anaandika Emmanuel Chengula…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Spika wa Bunge, mjini Dodoma imeeleza kuwa kufuatia kuwapo kwa muswada huo, Bunge la Jamhuri, limeanza kupokea maoni kutoka kwa wadau, kuanzia Ijumaa iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwisho kwa wadau kuwasilisha maoni yao, ni leo Jumapili, tarehe 7 Juni 2020.

Muswada unaohusu “Sheria ya Utekelezaji wa Haki na wajibu wa Msingi,” umeingia bungeni kwa njia ya “hati ya dharura.”

Binafsi, nimejipa muda wa kuusoma muswada huu kwa utulivu mkubwa. Nilichogundua ni mambo matatu makubwa:

Mosi, ndani ya taifa hili, kuna baadhi ya watu wanaonekana hawana nia njema na taifa letu na wanataka kuharibu taswira ya taifa.

Hii ni kwa sababu, ndani ya muswada, kumesheheni mapendekezo yanayoonekana kwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri. Ndani ya muswada kumesheheni vifungu ambavyo vinalinda viongozi badala ya taifa.

Kwa mfano, ndani ya muswada kumependekezwa kuwa ili mtu aweze kufungua kesi zinazohusu uvunjwaji wa haki za binadamu, zinazotajwa katika Ibara ya 12 hadi 29 ya Katiba ya Jamhuri, ni sharti mhusika ambatanishe kiapo kuidhihirishia Mahakama ni kwa kiasi gani mlalamikaji ameathiriwa na uvunjifu wa kifungu hicho.

Kwa maneno mengi, ni lazima mlalamkaji athibitishe binafsi, jinsi alivyoathirika.

Mathalani, aliyefungua kesi dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na aliyekuwa mbunge wa Chadema, katika jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe, ni lazima aseme kuwa Spika wa Bunge aliposema, “Mwambe arudi bungeni, alikiuka Katiba na kuthibitishia mahakama jinsi mlalamikaji alivyoathirika na uvunjifu huo wa Katiba.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma

Hii ni kinyume na Katiba ya Tanzania inayoelekeza wajibu wa kila raia wake wa kulinda na kutetea Katiba, ikiwamo uwapo wa haki za binadamu ziliongezwa katika katiba ili watu waishi kwa kufuata misingi ya haki.

Sheria hii kama itapitishwa inaua moja kwa moja kesi za haki za binadamu ambazo mara zote hutokea katika Ibara ya 12-29 ya Katiba.

Aidha, ikiwa muswada huu utapitishwa na Bunge na kuwa sheria, vyombo vya kiutawala, vitakuwa na uwezo wa kufanya vyovyote itakavyo, katika uvunjaji wa Katiba.

Vyombo hivyo – hasa serikali na Bunge – vitafanya hivyo kwa sababu, ni ngumu sana kwa mlalamikaji kuithibitishia mahakama kuwapo kwa uvunjaji wa Katiba, kabla ya chombo hicho hakijaruhusu kufunguliwa shauri hilo na kusikiliza.

Ndio maana kabla ya kuwasilishwa kwa muswada huu, mashauri ya aina hiyo, huitwa kesi zenye maslahi ya umma – Public Interest Cases.

Mapendekezo haya ya muswada, yanakiuka pia Katiba na kuifanya Katiba kuwa ni kitabu cha kawaida sana; na ambacho hakihitajiki kulindwa kwa wivu mkubwa kama ilivofanyika katika mashauri mbalimbali ya kikatiba.

Haijaishia hapo, muswada unapendekezwa Rais wa Jamhuri, Makamu wa Rais, Spika, Naibu Spika, Jaji Mkuu na hata Waziri Mkuu, badala ya kushitakiwa wao kwa makosa ambayo wanaweza kuwa wametenda, basi sasa atashitakiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika hali ya kawaida huwa tuna proper party na necessary party katika mashitaka, kuruhusu kumshtaki mtu mmoja, mfumo wa mashitaka unakuwa haujakaa sawa.

Si hivyo tu: Muswada huu, unaunda mihimili ya dola – Mahakama, Bunge na Serikali – kuwa vyombo vinaongozwa na Mungu au malaika, ambao watakuwa hawaguswi na sheria na wana mamlaka ya kutenda lolote.

Rais John Magufuli

Kupitia sheria itakayotokana na muswada huu, viongozi hao, sasa watakuwa na kinga ya kutowajibishwa kwa lolote wakatalalolifanya.

Mbili, muswada huu umekuja bungeni katika kipindi ambacho Rais wa Jamhuri na Spika wa Bunge, wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kuvunja Katiba.

Miongoni mwa mashitaka hayo, ni pamoja na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), aliyekuwa anamlalamikia Spika wa Bunge, Job Ndugai, kumtangaza kumvua ubunge.

Lissu alifungua shauri hilo Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam. Washitakiwa walikwua Spika wa Bunge na wenzake. Ilisajiliwa kwa Misc. Civil case Na 18 ya mwaka 2019.

Naye Zitto Zuberi Kabwe, alifungua shauri dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na wenzake. Kesi yake, ilisajiliwa mahakamani kama Misc Civil Cause Na 1 ya mwaka 2020.

Tulishazoea huko nyuma tukiona mihimili hii mitatu – Mahakama, Bunge na Serikali – ikiheshimiana, kwa maana ya kwamba Mahakama ikitafsri sheria, basi serikali inakwenda kupeleka mapendekezo bungeni namna ya kuendana na tasfri ya Mahakama.

Lakini kinachoshuhudia katika mswada huu, ni serikali kuaamua kuipinga Mahakama hadharani kwa kupeleka muswada unaopingana na maaamuzi ya Mahakama.

Ukisoma Ibara ya 4 ya Katiba inasema: “Kutakua na mihimili mitatu ya dola: Bunge ambalo litakuwa linatunga sheria, Mahakama yenye kazi ya kuitafsri sheria na Serikali yenye wajibu wa kuitekekeleza sheria.”

Tatu, muswada unazungumzia pia Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania Sura 425. Kwamba, ‘eti mswada unatoa marekebisho katika Kifungu cha 2 ili kuwezesha sheria hiyo kutoa msamaha kwa baadhi ya wanasheria kutopitia kwenye mafunzo ya shule ya sheria.

Huu ni ubaguzi wa wazi wazi kwani umelenga kwa wanasheria wa serikali tu, bila kuangalia sekta zingne.

Kwani lengo la kuanzisha shule ya sheria limekufa mpaka tuone hakuna umhimu wa kwenda kusoma?

Ni ukweli usiopingika siku za nyuma serikali ulishindwa kesi nyingi mahakamani kwa sababu watu wao/wanasheria wao hawakua wameivishwa na shule hiyo kwa sasa ni hoja kwa hoja kwa sababu nao wamepitia shule ya sheria ndio maana kigezo cha kuwa mwanasheria wa serikali lazima upite shule ya sheria na uwe umefauru.

Kigezo cha kuwa hakimu ama wakili wa kujitegemea lazima uwe umeivishwa na shule hiyo ya sheria na ukafaulu.

Najiuliza aliyetoa wazo hili sina hakika kama alisoma pale shule ya sheria akafaulu kama kifungu hiki kimetengenezwa kuwaokota wasiojiweza na wanaofeli pale shule ya sheria sawa, lakini kama kwa lengo la kuhakikisha mfumo wa haki jinai na haki madai unakua imara hakukua na haja ya kufanya mabadriko hayo yasiyo na tija zaidi ya kuharibu misingi ya sheria na maana ya kuwa na Law school of Tanzania

Kuhusu sheria ya maswala ya rais, inapendekezwa eti rais asishitakiwe mpaka atoke madarakani, kwa uelewa wangu kuna tofauti kubwa kati ya rais na rais mstaafu hadhi yao sio sawa, na kwanini tusbiri mtu astaafu ndio ashitakiwe.

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Je, ikitokea ametenda makosa mengi ya kikatiba na ya kiraia hatuoni tunatengeneza mtu atakae ng’ang’ania madarakani kwa hofu ya kushitakiwa?

Katiba yetu ipo wazi kabisa kwamba rais atashitakiwa kwa makosa ya madai kwa nini tusiache ibaki hivyo hivyo ili tusitengeneze madikiteta wanaolindwa na mfumo wa sheria zetu?

Muswada huu unataka kuwaandaa wananchi kuelekea wapi?

Sheria ya uendeshaji wa Mahakama, eti leo Jaji Mkuu, Majaji na maafisa wa mahakama waliojailiwa na mahakama wamewekwa Kinga dhidi ya matendo watakayo fanya wakati wakatekeleza shuguli zao.

Hivi tunafkri hawa watu ni semi God’s au maana wapo wanaopoteza mafile ya kesi na yasionekane tena wakiwekewa kinga nafkri tunaongeza janga Zito kuliko Sasa hivi ambapo matendo haya yanapungua kwa kuhofia kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Halafu manaa ya immunity/kinga inakufa, kama kila mtu atakuwa na kinga yaani sasa atafanya kwa nia ovu halafu hawajibishwi.

Tutegemee mamuzi ya ajabu ajabu kwa sababu mtu ana kinga kisheria ya kutoshitakiwa.

Kule Arusha kuna hakimu alishirikiana na mwanasheria mkuu wa serikali kuchoma faili, bahati nzuri serikali iliwakamata baadaye wahusika.

Ina maana kwa sheria hii ingelikuwa imepitishwa wasingekamatwa kwanini tunaandaa Miungu itakayoligharimu taifa.

Ni muhimu Watanzania zindukeni elezeni nchi yenu mnataka iwaje? Tunaanda Mambo magumu ya kuharibu nchi badala kuiboresha ili pawe sehemu salama ya kuishi.

1 Comment

  • Kulikoni mbona wataharibu katiba kwa maslahi yao na wao hawaongozi milele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!