Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kupotea kwa Mwandishi wahabari, THRDC yatua Kibiti
Habari Mchanganyiko

Kupotea kwa Mwandishi wahabari, THRDC yatua Kibiti

Pili Mtambalike, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (wakwanza) na Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)
Spread the love

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na wadau wengine wameunda kamati ndogo ya uchunguzi na kuituma Kibiti kuthibitsha taarifa zaidi za kupelekwa kusikojulikana mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Azory Gwanda, na kuweza kuzungunza na makundi mbalimbali, anaandika Nasra Abdallah.

Hadi sasa ni siku 18 zimepita tangu alipopotea Gwanda mnamo tarehe 21 November 2017 bila kuwepo kwa jitihada za kutosha za kumtafuta kutoka vyombo vya usalama.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam na waandiahi wa habari, Olengurumwa amesema sababu ya kuunda kamati hiyo ni katika kufatilia kinaga ubaga juu ya kupotea kwa Mwandishi huyo, mazingira ya kupotea kwake, sababu za kupotea, pamoja na jitihada zilizofanywa na polisi pamoja na Jamii inayomzunguka kuhakikisha anarudi.

Amebainisha kwamba, timu hiyo ilipewa hadidu za rejea iliweza kuonana na mke wa Azory na kupata historia yake, kuonana na ndugu jamaa na marafiki, majirani, serikali za mitaa, pamoja na Polisi na kuongeza kuwa engo la kuunda kamati hiyo ilikuwa ni kuepuka kufanyia kazi taarifa ambazo hatuna uhakika nazo.

Katika mahojiano hayo, Olengurumwa amesema mke wa Azory, Anna Penoni ameomba kupatikana kwa mume wake kwani ndio tegemeo lake na hana msaada mwingine.

“Kwa sasa mimi ni mjamzito na siku yoyote nitajifungua, mume wangu ndiye msaada mkubwa kwangu, naomba serikali isikie kilio changu mume wangu aweze kurudi akiwa salama”.

Wakati kwa upande wa Majirani wa Azory wamesema huenda Azory amekamatwa kutokana na kazi yake ya uandishi na wanaamini waliomchukua ni watu ambao mwisho wa siku watamrudisha kwakuwa hata wakati wanamchukua hakukuwa na viashiria vyovyote kuwa watu hao walikuwa na nia ya kumfanyia ubaya wowote.

Kwa upande wa viongozi wa serikali za mtaa anaoishi ndugu Azory, wamesema wao hawakuwa na taarifa zozote za kupotea kwa Azory mpaka pale mke wake alipowapa taarifa juu ya tukio hilo.

Hata hivyo viongozi wa mtaa walisema hawana wasi wasi na mwandishi huyo kwani amekuwa akipigania haki za watu wengi kwa muda mrefu na hivyo isingekuwa rahisi kwa mwandishi huyo kutekwa na watu wasiojulikana. Na wao pia wanaamini huenda yupo kwenye mikono salama na anaweza akaachiwa muda wowote.

Pia Polisi Mkoa wa Pwani kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, amekiri kupokea taarifa za tukio la kupotea Azory liliripotiwa katika kituo cha polisi Kibiti na kupewa RB No.Kibiti/RB/1496/2017.

“Hata hivyo kamanda huyo wa polisi amesema kwamba kwakuwa suala hilo tayari limesharipotiwa polisi wao wanandelea kulifanyia kazi na endapo watapata taarifa zitakazoweza kusaidia kupatikana kwake wataufahamisha umma na mke wake kwakuwa alishaacha mawasiliano yake katika kituo hicho cha polisi,” alielezea Olengurumwa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania ((MCT), Kajubi Mukajanga, amesema Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Waandishi Wanawake Tanzania (TAMWA; Umoja wa Waandishi wa Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (OJADACT), Umoja wa Vilabu vya Wanahabari Nchini( UTPC) pamoja na wadau wengine wa habari wanalaani kitendo cha kupelekwa kusikojulikana kwa mwandishi huyo.

Kupitia mkutano hio Mukajanga ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania vihakikishe kuwa kila raia anaishi kwa uhuru na usalama nchini Tanzania na Jeshi la Polisi liwe tayari kuwalinda raia na mali zao dhidi ya jambo lolote baya.

Pia amezishauri AZAKI, vyombo vya habari na umma wa watanzania kwa ujumla kuwa wanapaswa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vyovyote ambavyo vinalenga au kuashiria kuzuia uhuru wa maoni nchini Tanzania.

“Tunapaswa sote kukemea kwa sauti moja hali yoyote inayozuia kufurahia haki zetu.

Leo ni Azori na wengine haijulikani siku wala saa ya kutekwa au kupotea kwa mwandishi , mtetezi au raia wa kawaida hivyo Watetezi wa haki za binadamu tuungane na kupaza sauti zetu kwa pamoja juu ya hali hii ya watu kutoweka inayozidi kushika kasi chini.

Vilevile Mwenyekiti huyo amesema kutokan na wimbi hili la utekaji na kutoweka kwa Watanzania wenzetu, Serikali ya Tanzania inapaswa kutia sahihi na kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa kwa Ajili ya Ulinzi wa Watu Wote Waliotekwa na Kuwekwa Vizuini pamoja na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Utesaji na Vitendo Vingine vya Kikatili vinavyotweza utu wa Binadamu.

Kama vile haitoshi ametakaViongozi wa siasa na Bunge waone haja ya kulijadili suala hili la utekajji na kupotea kwa watanzania na kuja na maazimio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!