HOSPITALI ya Aga Khan imepewa jukumu la kupima virusi vya corona (COVID-19) kwa gharama ya Sh. 275,000 kwa Mtanzania. Anaandika Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).
Kwa wageni kutoka nje ya nchi, watatakiwa kulipa Sh. 360,000 ili kupata huduma hiyo.
Taarifa ya hospitali hiyo iliyotolewa leo tarehe 7 Januari 2021, imeeleza kupewa mamlaka hayo na Maabara ya Taifa.
Pia hospitali hiyo imepewa mamlaka ya kutoa cheti cha corona kwa niaba ya Wizara ya Afya.
“Kliniki itafunguliwa kuanzia saa 2:15 asubuhi mpaka saa 6:30 mchana (Jumatatu-Ijumaa) na saa 2:15 mpaka saa 5:30 asubuhi siku ya Jumamosi,” imeandika taarifa hiyo na kwamba, utaratibu huo utaanza tarehe 8 Januari 2021.
Je mvuja jasho atamudu kulipa sh 275,000? Yaani anayesafiri kutoka Tanga kwa basi hadi Mombasa nauli sh 10,000 halafu kupima korona sh 275,000?? Are we serious?
Kwa nini kazi hiyo ipewe hospitali ya binafsi tena ya matajiri? Serikali haina hospitali na wataalamu wanaoweza kazi hiyo kwa bei nafuu?