Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kumekucha CCM: Nani kupenya?
Habari za Siasa

Kumekucha CCM: Nani kupenya?

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi akirejesha fomu za kuwania Urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Spread the love

JUMLA ya makada 31 kati ya 32 waliochukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kugombea urais visiwani Zanzibar, wameanza kuingizwa kwenye tanuri. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hussein Ibrahim Makungu, ndio kada pekee aliyetangaza ‘kukimbia’ tanuri hilo baada ya kueleza kutoa jina lake kwenye mbio za kumrithi Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar anayemaliza muda wake.

Mchakato wa kuchuja majina hayo umepanga kuanzwa leo tarehe tarehe 1 Julai 2020 mara baada ya kufungwa kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu pamoja na utafutaji wadhamini. Mchakato huo ulianza tarehe 15 Juni 2020 na kufungwa tarehe 30 Juni 2020.

Kwa Tanzania Bara, mchakato huo ni rahisi kwa kuwa, aliyejitokeza ni mgombea mmoja tu – Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa CCM Taifa – anayetetea nafasi yake kwa awamu ya pili.

Jecha Salum Jecha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akichukua fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na CCM, vikao vitakavyoanza ni vya uchujaji watia nia ya kugombea urais Zanzibar, ambavyo vitaanza leo na kufika kikomo tarehe 10 Julai 2020, baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea nafasi hiyo.

Lakini pia siku hiyo, NEC itapendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM, majina matatu ya wanachama wanaoomba kugombea urais wa Tanzania.

Ratiba ya CCM inaeleza kuwa, baada ya kikao cha NEC, Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika tarehe 11 hadi 12 Julai 2020,  utathibitisha jina la mgombea Urais wa Zanzibar, pamoja na  kuchagua jina moja la mgombea wa Urais wa Tanzania, kutoka majina yasiyozidi matatu, yatakayopendekezwa kwake na halmashauri hiyo.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akipokea fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

Michakato hiyo itatanguliwa na vikao vya uteuzi wa wagombea, ambapo Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC ya Zanzibar, itafanya mkutano wake kwa siku mbili, leo na kesho Alhamisi tarehe 2 Julai 2020.

Baada ya kikao cha sekretarieti ya kamati hiyo, tarehe 3 Julai 2020 Kamati ya Usalama na Maadili Zanzibar itafanya kikao chake.

Huku Kamati Maalum ya NEC ya Zanzibar, itaketi tarehe 4 Julai mwaka huu, kwa ajili ya kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kuhusu wanachama wanaoomba nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Tarehe 6 hadi 7 Julai, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itafanya kikao chake, kisha kufuatiwa na Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa, kitakachofanyika tarehe 8 Julai 2020.

Baada ya vikao hivyo, tarehe 9 Julai 2020 Kamati Kuu ya NEC itaketi kwa ajili ya kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa NEC, juu ya majina ya wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Urais wa Tanzania, na majina ya wanachama wasiozidi watatu wanaoomba kugombea urais wa Zanzibar.

Tarehe 10 Julai 2020, NEC itachagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea urais wa Zanzibar na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa, majina ysiyozidi matatu ya wanachama wanaoomba kugombea Urais wa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!