Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea: Sitanii, hili nitafanya Kinondoni
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea: Sitanii, hili nitafanya Kinondoni

Saed Kubenea, mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya ACT Wazalendo
Spread the love

SAED Kubenea, mgombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam mesema miongoni mwa mambo ambayo atayasimamaia hadi kufanikiwa kwake ni suala la kutoa mikopo kwa vijana pamoja na mbinu za ‘kutumia pesa kuzalisha pesa.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kubenea ametoa kauli hiyo leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020 kwenye Viwanja vya Buibui jijini humo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Akizungumza kwenye mkutano wake amesema, kipaumbele cha kwanza ni uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo, ambazo atazitumia kutoa mikopo pamoja na kuwajengea uwezo wananchi kuzalisha pesa.

“Nataka kuboresha mfuko wa bunge na kutoa zaidi ya asilimia 80 ya fedha kwa ajili ya kuboresha masilahi ya wananchi wa Kinondoni, nitatoa mikopo na kuwapa elimu ya ujasiriamali wananchi,” amesema Kubenea.

Amesema, jambo la pili ni utatuzi wa changamoto ya mafuriko kwa kupanua Mto Msimbazi na Mto wa Ng’ombe, kwa kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kwa wafadhili.

“Nataka kutoa kero ya mafuriko na bahati nzuri, fedha zipo za kupanua Mto Msimbazi na kuubadilisha kuwa kivutio cha utalii, Benki ya Dunia ilitaka kutoa fedha lakini haijatoa sababu serikali inasusua tunataka kuchukua halamshauri ili suala hilo likawe historia,” amesema Kubenea.

Ahadi ya tatu aliyoitoa mbele wa wananchi na wanachama waliohudhuria mkutano wake ni ujenzi wa Shule ya Kidato cha Tano na Sita, ili kuondoa kero kwa wanafunzi kwenda kutafuta elimu katika majimbo jirani.

“Halmashauri ya Kinondoni haina shule ya Kidato cha Tano na Sita. Tunataka tujenge shule ili watoto wetu wasiende mbali kutafuta elimu,” amesema Kubenea.

Pia ameahidi utatuzi wa changamoto ya uchafu wa mazingira kwa kuifanya kuwa fursa ya kiuchumi kwa kuanzisha kiwamda cha uchakataji taka kuwa mbolea.

Kubenea amesema, ujenzi wa kiwanda hicho utasaidia kuzalisha ajira kwa wananchi na kufanya mazingira kuwa safi na salama.

“Nataka tugeuze taka kuwa ajira sababu ukitengeneza taka kuwa mbolea utaajiri watu. Nitaanzisha kiwamda cha taka,” ameahidi Kubenea aliyekuwa mbunge wa Ubunge kupitia Chadema kati ya 2015-2020.

Akijinadi katika mkutano huo, Kubenea amewaomba wananchi wa Kinondoni wamchague kwa kuwa anauzoefu na kazi za bunge lakini pia ni mwanasiasa muaminifu asiyenunulika.

“Ninalifahamu bunge vizuri na nafahamu kazi za mbunge, nimekuwa mbunge mniamini sinunuliki, sina bei naahidi kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa. Sitababaishwa na kauli za rejareja wala kauli za uongo. Ukichagua mbunge ambaye anajua kazi za mbunge, anajua maana ya mbunge maendeleo katika maeneo yenu yatapatikana kwa haraka sana,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema, amemua kugombea Ubunge Kinondoni ili asimamie maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

“Ndugu zangu wa Kinondoni, mimi nataka kuwa mbunge wa Kinondoni ili nisimamie maendeleo na masilahi ya wananchi wa Kinondoni,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema, “Kuna tofauti ya mbunge anayetokana na wananchi na anayetafuta ubunge kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na mbunge anayekwenda kutumikia chama chake na baishara zake, hiyo tofauti lazima muielewe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!