Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea: Sio viwanda tu, nyumba za serikali zirejeshwe
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea: Sio viwanda tu, nyumba za serikali zirejeshwe

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo (Chadema), ameitaka serikali kurejesha nyumba za serikali zilizouzwa kiholela na si viwanda vilivyobinafsishwa pekee. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akichangia bungeni Bajeti ya Waziri Mkuu ya Mwaka wa Fedha 2019/20 leo tarehe 9 Aprili 2019 mbunge huyo amesema, Rais John Magufuli ameonesha nia njema ya kutaka viwanda vilivyobinafsishwa kwa mikataba mibovu na ambavyo haviendelezwi, virejeshwe serikalini.

Amesema, kwa kasi hiyo hiyo ya kurejesha viwanda vilivyobinafsishwa iende sambamba na urejeshwaji wa nyumba za serikali zilizouzwa kiholela.

“Nimemsikia rais anasema kwamba, viwanda vyote vimebinafsishwa na serikali, na wale waliopewa kazi ya kubinafsisha viwanda hivyo hawakuviendeleza, wavirudishe serikalini.

“…na akaomba radhi kwa niaba yake binafsi, na kwa niaba ya watangulizi wake kwa mambo ambayo yalifanyika katika nchi juu ya uuzaji na ubinafsishaji wa mali za serikali,” amesema Kubenea.

Hata hivyo amesema, Rais Magufuli amesahau jambo moja muhimu kwamba, kuna nyumba za serikali zilizouzwa kiholela, nazo zinahitajika kurejeshwa.

“Lakini mheshimiwa rais amesahau jambo moja kubwa sana ambalo limefanyika katika nchi hii, nyumba za serikali zilizouzwa rais hajasema zirejeshwe.

“Tunaomba nyumba zote za serikali zilizouzwa kiholela na kienyeji, zirejeshwe mikononi mwa umma,” amesema.

Mbunge huyo wa Ubungo amefafanua kwamba, nyumba zote ziliuzwa kiholela zinapaswa kurejeshwa serikalini kwa kuwa, zilifujwa kama ilivyo viwanda.

Katika mchango wake Kubenea amesema, serikali haiwezi kutekeleza bajeti yake licha ya kujinasibu kuwa inafanya vizuri.

“Ukisoma mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/18 ambayo sasa tunaelekea kuadaa bajeti mpya, unakuta katika mwaka wa fedha wa 2017/18 serikali ilikusanya takribani sh tilioni 17 .9 na matumizi ya serikali yalikuwa tilioni 18.7 kwa mujibu wa Kitabu cha Hotuba ya Waziri Mkuu.

“Sasa kama mapato yalikuwa tilioni 17.9, matumizi yakawa tilioni 18.7 maana yake ni kwamba nakisi ya bajeti yetu ilikuwa inakaribia karibu sh. 1 Trilioni,” amesema na kuongeza;

“Na hiyo ama ipatikane kutokana na mikopo ama misaada kutoka nje, sasa matokeo yake bajeti imeshindwa kutekelezwa.”

Amesema, ukisoma bajeti yote, mishahara na matumizi mengine ya serikali yamefikia karibu bajeti ya fedha zote zilizokusanywa, kwamba fedha zimetumika katika kulipa mishahara na matumizi mengine ya madeni ya serikali.

“Sasa serikali isiyoweza kufikia malengo ya makusanyo yake, haiwezi kutekeleza bajeti yake kikamilifu.

“Sh. 6 trilioni ambayo zilitengwa kwa ajili ya maendeleo, hizi zote maana yake hazipo katika makusanyo ya serikali,” amesema Kubenea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!