Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea: Nilihofia kugawa kura Ubungo
Habari za Siasa

Kubenea: Nilihofia kugawa kura Ubungo

Spread the love

SAED Kubenea, mgombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, amesema hakugombea ubunge katika Jimbo la Ubungo ili kutogawa kura za upinzani. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani kwenye Kata ya Tandale, jimboni humo Mohammed Ismail, tarehe 13 Septemba 2020 amesema, hayupo radhi kugawa kura za upinzani.

”Nimefikia uamuzi wa kuacha kugombea Ubungo kwasababu  ningeng’ang’ania kugombea, ningegawa kura na hatimaye CCM ishinde, sitaki kushiriki dhambi hiyo,” amesema Kubenea na kuongeza:

“Nimegombea Kinondoni kwa kuwa, naijua vizuri na nimeshiriki shughuli nyingi nikiwa kwenye Manspaa ya Kinondoni kwa mwaka mmoja na nusu.”

Amesema, ataendelea kutetea ajenda za wananchi na kwamba atahakikisha anamaliza athari za mafuriko katika jimbo hilo.

Amesisitiza kwamba, licha ya kufanyiwa vitimbi na hata kumwagiwa tindikali usoni wakati akiwatetea wananchi kupitia kalamu yake, hajawahi kuusaliti umma.

1 Comment

  • “Разум, однажды расширивший собственные границы, никогда не воротится в бывшие.” – доказывал А. Эйнштейн. Превеликое спасибо только за то, что Вы, своими заметками, позволяете разуму перейти за пределы привычных границ.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!