MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ameahidi kutoa Sh. 14 milioni kwa ajili ya kujenga kivuko kilichoosombwa na mafuriko kilichopo Mabibo Sahara. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea).
Kubenea ametoa ahadi hiyo leo alipotembelea eneo hilo kusikiliza kero za wakati hao wa Mabibo Sahara zikiwemo na kivuko hicho cha waenda kwa miguu ambacho kilisombwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
Wakati wa maeneo hayo wamekuwa na kero ya kuvuka katika eneo hilo baada ya madaraja mawili kusombwa na maji, kabla ya kikundi cha vijana kujenga daraja la magogo ambalo wananchi wanalipia sh 200 ili kupita.
Mbali na ahadi hiyo, mbunge alitoa kiasi cha sh 150,000 ili vijana hao wawaruhusu wananchi kupita bure kabla ya kujenga kivuko hicho kwa kiwango kama ilivyokuwa hapo awali.
Hata hivyo mbele ya mbunge kuliibuka mabishano kati ya wananchi kwa kila mmoja akitaka daraja lijengwe eneo ambalo yeye anaona sahihi. Mgogoro huo ulimalizwa na Kubenea kwa kuwaahidi wataalamu kutoka manispaa watafika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu ili kujua eneo sahihi la daraja linatakiwa kujengwa wapi.
Fatma Said mwananchi wa eneo hilo ambaye alimwelezea mbunge umuhimu wa kuhamisha daraja hilo kwenda katika eneo lingine lisilo na makazi ya watu.