Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea aanza safari ya kukabiliana na Tarimba
Habari za Siasa

Kubenea aanza safari ya kukabiliana na Tarimba

Saed Kubenea
Spread the love

MGOMBEA ubunge katika jimbo la Kinondoni, kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Saed Kubenea, amepanga kufungua kampeni zake za kuwani nafasi hiyo, kesho Jumapili, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Kinondoni … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mratibu wa uchaguzi wa ACT- Wazalendo, katika jimbo la Kinondoni, Leila Madibi, mkutano wa kumnadi Kubenea, utafanyika kwenye viwanja vya Buibui, vilivyopo Mwananyamala.

Leila anasema, mgombea wao amechelewa kufungua kampeni zake, kutokana na matatizo mbalimbali, ikiwamo kufunguliwa kesi ya jinai, mkoani Arusha.

Amesema, “kesho ndio tunaanza mchakamchaka wa siku takribani 35 za kutafuta uungwaji mkono wa wananchi wa Kinondoni,” ameeleza Leila ambaye alikuwa diwani katika Manispaa za Kinondoni, Ubungo na jiji la Dar es Salaam, kati ya mwaka 2015 na Juni 2020.

Anaongeza, “ni kweli kuwa tumechelewa kufungua kampeni zetu. Lakini tunaamini kwa aina ya mgombea tulienaye na kukubalika kwa chama chetu, tutashinda uchaguzi huu.”

Leila anasema, katika kampeni hizo, mgombea wao amepanga kufanya kampeni zake kwa kwenda nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na mtu kwa mtu, ili kuwashawishi wananchi wamchague.

Amesema, “Kubenea anafahamika. Anauzika. Anazo sifa zote za kuwa mbunge na kuwakilisha wananchi. Wengi wanamfahamu kutokana na kazi zake kwa jamii na ujasiri wake wa kutetea wananchi. Hivyo basi, tunaamini hatujachelewa.”

Mbali na uzinduzi wa kampeni hizo za kuwania ubunge, mkutano huo utakaohudhuliwa na kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe, unatarajiwa kueleza kile kinachoitwa, “makubaliano ya ushirikiano wa kimya kimya, kati ya ACT- Wazalendo na Chadema.”

Katika siku za karibuni, Zitto amekuwa akieleza kuwa chama chake na Chadema, wamepanga kushirikiana kwa kusimamisha mgombea mmoja wa urais, ambapo ACT- Wazalendo, kitamuunga mkono Tundu Lissu, mgombea urais wa Chadema.

Kuhusu athari za kuchelewa kwa kampeni hizo, Leila anasema, haoni kuwa kuna shida kwa kuwa jimbo la Kinondoni, linafikika kwa urahisi na mgombea wao, bado anaweza kufikia wapigakura kokote waliko.

Katika uchaguzi huu, Kubenea ambaye amepata kuwa mbunge wa Ubungo, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika uchaguzi mkuu uliyopita, anakabiliana na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abasi Gulamhussen Tarimba.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo anajivunia rekedi yake ya uwakilishi bungeni na uwezo wake wa kuangusha vigogo, ambapo mwaka 2015, alimshinda aliyekuwa meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!