Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea awapa pole waliopatwa na maafa ya mvua
Habari za Siasa

Kubenea awapa pole waliopatwa na maafa ya mvua

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea, jana aliungana na mamia ya wananchi wa Kata za Kimara na Makuburi, kutoa pole kufuatia msiba wa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shule ya Sekondari Makoka, Rashid Charu Makoye. Anaripoti Mwandishi wetu… (endelea).

Mwanafunzi huyo alifariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati alipokuwa akivuka mto Gide, majira ya asubuhi. Mwanafunzi huyo alikuwa akielekea shuleni kwenye masomo yake.

Taarifa zinasema, Rashidi ni mkazi wa Mbezi Makabe na kwamba alisombwa na maji katika eneo la Makoka na Kimara Baruti.

Kubenea alifika eneo hilo majira ya saa nane mchana na kulakiwa na mamia ya wananchi waliokuwa wamejiukusanya kupokea taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na hatua zilizochukuliwa.

Akizungumza mbele ya kadamnasi akiongozwa na mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makoka, Mzee Akyoo, mbunge huyo alisema, analifahamu tatizo la kivuko kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo.

Kubenea alisema, tokea alipofika hapo miaka miwili iliyopita kwa lengo la kukutana na wananchi kutafuta suluhu ya kudumu la tatizo hilo, aliliwakilisha jambo hilo kwenye vikao vya halmashauri na kuahidiwa kuwa daraja la waendao kwa miguu litajegwa, tena haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo, Kubenea amesema, ni jambo la kusitikisha kuona ahadi hiyo iliyotolewa na serikali haikutekelezwa mpaka sasa.

“Kutokana na kutotekelezwa kwa ahadi na mipango ya serikali kuchukua muda mrefu, nimeamua kupitia fedha za mfuko za Jimbo, kujenga daraja la muda. Katika hatua ya sasa, nitaekeleza mainjinia wa manispaa kufanya kufanya tathimi ya gharama za mradi huu ili fedha hizo ziweze kutolewa,” alisisitiza Kubenea.

Akaongeza, “naomba tuvumilie na yaliyotokea tumuachie Mungu. Lakini ninawaahidi kwamba sitamaliza miaka yangu mitano, bila kulipatia ufumbuzi jambo hili.”

Kwa mujibu wa Kubenea, manispaa ya Ubungo ambayo yeye ni mjumbe wa vikao vya maamuzi, ilitenga kiasi cha Sh.30 milioni kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo na kwamba fedha hizo zimepelekwa Tarura kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!