Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea awaibua Tundu Lissu, Ben Saanane, Ulimboka bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea awaibua Tundu Lissu, Ben Saanane, Ulimboka bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ameibua bungeni tukio la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Mwanahabari Absalom Kibanda, Ben Saanane na Dk. Steven Ulimboka, akiitaka serikali kueleza lini itakamilisha uchunguzi wa matukio hayo. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akiuliza swali bungeni jijini Dodoma leo tarehe 14 Septemba 2018, Kubenea alihoji ni lini serikali itakamilisha uchunguzi wa matukio ya kihalifu yanayofanana na ugaidi ambayo wamekuwa wakifanyiwa watu mbalimbali na kuleta ripoti bungeni.

Vile vile, Kubenea alihoji serikali ina mpango gani wa kushikika wa kulinda raia wenye msimamo kali katika kukosoa serikali, hasa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wanahabari, kama inavyolinda viongozi wake.

“Wananchi ambao wameumizwa, wametekwa, wamepotea si suala la kuimarisha vituo vya polisi kwenye ulinzi shirikishi, kwa kuwa sasa serikali inalinda viongozi wake wakuu hailindi na angani, baadhi ya wananchi hasa waliokuwa na msimamo mkali wa kukosoa serikali, kama waandishi wanaharakati na wana siasa upinzani. Je serikali, ina mpango gani wa kushikika wa kulinda raia hawa waliojitolea kutetea nchi yao kwa masilahi ya watanzania wote?” Amehoji Kubenea.

Akijibu maswali ya Kubenea, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, amesema vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa matukio hayo, hata hivyo, kuna baadhi ya matukio uchunguzi wake umekwama kutokana na baadhi ya watu kutotoa ushirikiano.

“Zipo kesi nyingine zinaendelea kuchunguzwa. Nitoe wito kwa watu husika kutoa ushirikiano, mara nyingi tumekuwa tukitaka ushirikiano kutoka kwenye chama anachotoka, lakini chama hicho kimekuwa kikimzuia dereva ushirikiano ni muhimu katika kukabiliana na kuharakisha uchunguzi,” amesema.

Kuhusu swali la wanasiasa kupatiwa ulinzi, Masauni amejibu kuwa, serikali kupitia Jeshi la Polisi imekuwa ikilinda raia pasipo matabaka

“Kwanza kabisa nataka nichukue fursa hii kumpinga na kumkosoa vikali Kubenea kutokana na utangulizi wa swali lake alilouliza, kimsingi serikali kupitia jeshi la polisi imekuwa ikilinda raia na mali zao, hakuna matabaka,katika kusimamia raia na mali zao hiyo ndio kazi ya Jeshi la Polisi kila siku, kusema kuna watu wanakosoa serikali hiyo ni kauli potofu na si sahihi, nadhani mwenyekiti kwa mamlaka yako ungefuta katika answerd sababu ni upotoshaji mkubwa kwa jamii,” amejibu Masauni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!