MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika jimbo la Ubungo, leo Jumapili, tarehe 20 Oktoba, aliungana na mamia ya wananchi katika kutafuta mwili wa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shule ya Sekondari Makoka, Rashid Charu Makoye. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).
Mwanafunzi huyo alitoweka tangu siku ya Alhamisi baada ya kusombwa na maji wakati alipokuwa akivuka mto Gide, mpkani mwa mtaa wa Kimara Bauti, kata ya Kimara na Makoka, mtaa wa Makuburi.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili asubuhi, wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akielekea shuleni kwa ajili ya masomo yake.
Akiwa na baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wameongoza na mbwa maalum wa kutafuta miili ya watu waliopatwa na maafa kama kusombwa na maji na kufukiwa na kifusi, Kubenea alitumia nafasi hiyo kuwapa pole ndugu wa kijana huyo na kuwaeleza kuwa yuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
https://youtu.be/v_NU-uWRRXY
Kwa mujibu wa familia yake, Rashidi ni mkazi wa Mbezi Makabe na kwamba tokea siku alipotumbukia kwenye mto huo kumekuwa na jitihada za kumtafuta, zikiongozwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Makoka, Emmanuel Benjamin Akyoo na mbunge huyo.
Kubenea alifika eneo hilo majira ya saa nane mchana na kulakiwa na mamia ya wananchi waliokuwa wamejiukusanya kupokea taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na hatua zilizochukuliwa.
Leave a comment