Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea ateta na Bawacha
Habari za Siasa

Kubenea ateta na Bawacha

Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amewataka viongozi wa Baraza la Wanawake wa Chdema (Bawacha), jimbo la Ubungo, kukitetea na kulinda chama chao kwa gharama yeyote ile kwa kuwa wanawake hao, ndio nguzo muhimu ya chama hicho, anaandika Mwandishi Wetu.

Ametoa kauli hiyo leo jioni katika ofisi za Chadema kata ya Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hiko cha ndani mbunge huyo aliwasihi wanawake kukilinda chama chao, kulinda mafanikio yaliyopatikana hasa katika uchaguzi mkuu uliopita na kukitetea ili kkuhakikisha kinaingia Ikulu mwaka 2020.

Amesema,” mafanikio haya tulioyapata siyo haba, ingawa tulistahili kupata makubwa zaidi. Naomba tuyalinde na kuhakikisha tunapata mafanikio makubwa zaidi.”

Akizungumza kwa hisia kali, Kubenea amesema, wanawake ni watu muhimu katika ukuaji wa chama na udumishaji wa demokrasia.

Hivyo basi, aliwataka kuendelea na moyo huo kwa ustawi mpana wa chama hicho na taifa.

“Wanawake ni watu muhimu sana hasa katika ukuaji wa demokrasia ya nchi hii. Nawaombamzidi kuendelea kuwa na mshikamano huo huo na kuwa wamoja,” amesema Kubenea.

Kwa mujibu wa Kubenea, Chadema kimekuwa kwa kasi ndani ya miaka miwili iliyopita, lakini kasi hiyo inakabiliwa na changamoto ya kuogopwa na Chama Cha Mapinduzi na hivyo, kuvitumia vyombo vya dola kukiandama.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa Kinondoni, Suzan Lymo na Mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Kinondoni, Magreth Mugyabuso.

Viongozi hao kwa pamoja waliahidi kutoa ushirikiano kwa mbunge na wanawake wote ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwa imara.
Kubenea yupo katika ziara ya kichama ya siku 14 kwa lengo la kuimarisha chama.

Kesho Jumatano ataendelea na ziara yake katika kata ya Kimara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!