May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea ajitabilia ushindi asilimia 52

Spread the love

MGOMBEA Ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo, Saed Kubenea amesema anatarajia kushinda uchaguzi wa jimbo hilo kwa wastani wa asilimia 52.8 hadi 58.2. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kubenea ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 26 Oktoba 2020 wakati anazungumza na wanahabarii jijini Dar es Salaam, kuhusu mwenendo wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni.

“Tuna uwezo wa kushinda uchaguzi huo ikiwa wapiga kura watakuwa kati ya wapigakura 160,000 na chini ya 200,000 kati ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura 253,000.”

“Sisi tuna amini, tutashinda kati ya asilimia 52.5 na 58.2 kama uchaguzi huo utakua huru na haki,” amesema Kubenea.

Hata hivyo, Kubenea amesema, ushindi utakuwa mwembamba kutokana na hatari ya kugawana kura kati yake na Mgombea Ubunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Susan Lyimo.

Saed Kubenea, Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

Kubenea amesema, ana uhakika wa kushinda uchaguzi huo kutokana na mpinzani wake wa karibu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Tarimba hakubaliki kwa wananchi wa Kinondoni.

“Tuna uhakika wa kushinda na kwa sababu mgombea wa CCM hakubaliki. Hana watu, amezungukwa na genge la kina madenge CCM, wenyewe wanalalamika chama hakipo kimegawanyika. Hana mizi chini,” amesema Kubenea.

Amesema, wananchi wa Kinondoni wanahitaji mtu anayefanana nao na kwamba yeye ana sifa hizo.

“Wananchi wa Kinondoni wanahitaji kuona mtu ambaye wanalingana kimaisha. Wakati wananchi wa Kinondoni wanazama kwenye maji yeye anakaa ghorofani.”

“Wakati wananchi wanaishi na shida ya maji yeye anakaa ghorofani. Kinondoni inahitaji mtu anayefanana na shida zao na huyo sio mwingine wananiona ni mimi Saed Kubenea,” amesema Kubenea aliyekuwa Mbunge wa Ubunge kupitia Chadema kati ya mwaka 2015-2020

Kubenea amesema, ana uhakika wa kushinda kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni na jiji la Dar es Salaam wanafahamu namna wabunge wa vyama vya upinzani walivyopigania masilahi yao.

“Pia, wakati halmashauri iko Ukawa tulisimama kidete wananchi waliobomolewa nyumba zao walipwe fidia. Hivyo, wananchi wanajua wabunge wa CCM hawakuchukua juhudi zozote kuishauri Serikali iwalipe wananchi,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema, ana uhakika wa kushinda kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni na Jiji la Dar es Salaam wanafahamu namna wabunge wa vyama vya upinzani walivyopigania masilahi yao.

“Pia wakati halmashauri iko Ukawa tulisimama kidete wananchi waliobomolewa nyumba zao walipwe fidia. Hivyo, wananchi wanajua wabunge wa CCM hawakuchukua juhudi zozote kuishauri Serikali iwalipe wananchi,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema, “wananchi wanajua mpinzani wetu CCM iliongoza Kinondoni tangu nchi ipate uhuru lakini haina shule ya kidato cha tano na sita.”

“Wananchi wanajua katika huduma zetu ya sekta  ya afya sio nzuri imefikia hatua mwili wa marehemu huwezi kuuondoa bila kuulipia. Mama mjazito akifanyiwa operesheni analipa.”

Mwanasiasa huyo amesema, sababu nyingine itakayomfanya ashinde uchaguzi huo, ni kufanikiwa kwake kuwafikia wananchi katika maeneo yote, licha ya kuchelewa kufanya kampeni.

“Mimi nitashinda kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kazi kubwa ambayo tumeifanya katika kampeni ambapo kwa muda mchache tumefanikiwa kufika kata zote 10 na mitaa 51 ya jimbo la Kinondoni,” amesema Kubenea.

Amesema katika kampeni zake alifanikiwa kufikisha sera zake kwa wananchi wa jimbo hilo.

“Tumeweza kuwasilisha hoja zinazowakabili wananchi wa Kinondoni ikiwemo suala la mafuriko na Mungu hua si athumani alileta baraka mbaya siku moja kwa kuleta mafuriko Dar es Salaam,  wananchi wakaona wakakumbushwa juu ya adha ya mafuriko. Tulipoenda zungumza nao walikuwa ni mashahidi wa jambo lililowaathiri wakati wa uchaguzi,” amesema Kubenea.

error: Content is protected !!