Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea aishiwa uvumilivu, kutinga kwa msajili wa vyama vya siasa
Habari za Siasa

Kubenea aishiwa uvumilivu, kutinga kwa msajili wa vyama vya siasa

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea amesema anatarajia kumwandika barua Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kutokana na kuzuiliwa kufanya shughuli zake za kijimbo katika Jimbo lake. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Miongoni mwa shughuli zake alizozitaka kuzifanya hivi karibuni ni pamoja na kuwaelezea wananchi juu ya ujenzi wa Daraja katika mto Gide lililopo katikati ya Makoka na Kimara Baruti  ambapo mvua zilizonyesha juzi zilileta maafa na mtoto ajulikanae Rashid Makaye alitumbukia katika daraja hilo namwili wake kushindwa kuonekana hadi leo.

Akizungumza leo tarehe 20 Oktonba 2019, jijini Dar es Salaam wakati wa ugawaji wa mihuli ya Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA )katika jimbo lake,alisema atamwandikia barua msajili huyo na kumuambatanishia  barua zote za polisi na video za juzi alizozuiliwa asifike katika Mkutano wake na wananchi.

Pia amesema anapeleka barua kwa Spika wa Bunge rasmi Job Ndugai ili awasilishe malalamiko yake  kwa  Rais,John Magufuli .

“Kama  madai haya hayatasikilizwa nitakishawishi Chama change cha CHADEMA  kiandike malalamiko rasmi  kwenye Jumuiya ya Kimataifa,” alisema na kuongeza;

“Ni kweli tumechoka kuzuiliwa huku kwa mikutano haya tunayofanyiwa yamepitiliza na kudhoofishwa juu zangu za kuwaletea maendeleo wananchi katika jimbo langu…… licha ya yote ninayopitia nawaambia kuwa Ubungo nimejipanga nakuhakikisha tutapata wagombea wa nafasi zote na tutashida,” amesema.

Aidha, alisema anaamini kuwa anazuiliwa kufanya mikutano katika jimbo lake kwa sababu yeye ni miongoni mwa wabunge wanaofanya kazi kubwa ndani ya kipindi kifupi ya kuwatumikia wananchi na kuwapelekea maendeleao.

“Nimetumia fedha ya mfuko wa jimbo kuwapatia maendeleo wananchi wa jimbo langu kwa kuwawezesha baadhi ya vikundi vya vijana na wakinamama kuwapatia fedha za kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo,’’ amesema na kuongeza.

“Mfuko ulitoa Milioni nane kwa ajili ya kujenga kisima katika Shule ya msingi Mabibo na kutoa Milioni 12 kwa ajili ya uchimbaji wa kisima katika soko la Gamesi lilipo Mabibo ili wafanyabiashara wa soko hilo wapate maji,” amesema.

Wakati huo huo, Kubenea aligawa mihuri 46 ya mitaa yote ya jimbo lake ambayo itatumika katika ujenzi wa chama na kwenye Uchaguzi wa Serikali ya Mitaa ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni.

“Nagawa mihuri hii kwa jimbo zima na hii mihuri inafanana yote na ugawaji huu ni dharula kutokana na moja ya vipengele vilivyopo katika uchaguzi wa mwaka huu wa serikali ya mitaa ya kutaka mgombea kuwa na muhuri wa mdhamini wa ngazi ya chini ya chama ambayo ni tawi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!