Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Kubenea asikitishwa na mlundikano wanafunzi
Habari za Siasa

Mbunge Kubenea asikitishwa na mlundikano wanafunzi

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, akizungumza na uongozi wa shule ya msingi Kawawa, iliyopo Kata ya Mabibo
Spread the love

SAED Kubenea Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaama, amesikitishwa na kuwapo msongamano wa wanafunzi katika shule ya Msingi Kawawa, anaandika Faki Sosi.

Msongamano huo unatokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.

Kubena akiwa katika shule hiyo iliyopo kata ya Mabibo, alishuhudia msongamano wa wanafunzi shuleni hapo ambapo wanafunzi 3100 ambao wanatumia vyumba 32 wakati mahitaji ni vyumba 64.

Mbunge huyo alifika katika shule hiyo baada ya kuombwa na uongozi wa kamati ya shule kuja kuangalia sehemu litakapojengwa jengo la utawala wa shule hiyo na kusikiliza kero mbalimbali.

Mbunge huyo akizungumza na kamati ya shule, aliahidi kuchangia gharama za chakula kwa ajili ya wafanyakazi watakaofyatua matofali ili kurahisha ujenzi wa jengo hilo.

Wanafunzi wa darasa la saba wakiwa darasani

Wakati huo huo Kubenea ameushari uongozi wa shule kuangalia uwezekano wa kujenga majengo ya ghorofa ili kukabaliana na uhaba wa maeneo.

Katika ziara hiyo, Kubenea alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa darasa la saba wanaojiandaa na mitihani yao ya taifa na kuahidi kuwalipia ada watoto watatu wa kwanza watakaofaulu mitihani yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!