Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Korea Kusini yaijaribu Korea Kaskazini
Kimataifa

Korea Kusini yaijaribu Korea Kaskazini

Moon Jae, Rais wa Korea Kusini
Spread the love

KOREA Kusini inasema kuwa kuna dalili kuwa Korea Kaskazini inapanga majaribio zaidi ya makombora yanayokwenda masafa marefu, anaandika Mwandishi Wetu.

Maofisa wa ulinzi wamekuwa wakilishauri bunge mjini Seoul baada ya Korea kulifanyia jaribio bomu la nyuklia mwishoni mwa wiki.

Korea Kusini imejibu kwa kufanya majaribio kwa kurusha makombora kwa kutumia ndege na kutoka ardhini.

Marekani imeonya kuwa tisho lolote kwake na kwa washirika wake litajibiwa na jeshi la nchi hiyo.

Korea Kusini inasema kuwa ililifanyia majaribio bomu la haidrojeni ambalo linaweza kuwekwa kwa kombora la masafa marefu.

Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura baadaye leo kujadili hatua za kuchukua.

Chang Kyung-soo, ambaye ni Ofisa  kutoka wizara ya ulinzia aliliambia bunge, “tunaendelea kuona dalili za uwezekano wa makombora zaidi ya masafa marefu. Pia tunaweza kutabiri kuwa Korea Kaskazini huenda ikarusha kombora la masafa marefu.

Wizara hiyo pia ililiambia bunge kuwa huenda Marekani ikapeleka manowari wa nyuklia ya kubeba ndege katika rasi ya Korea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!