Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Korea Kaskazini yaelekeza kombora Japan
Kimataifa

Korea Kaskazini yaelekeza kombora Japan

Mifano ya makombora ya Scud yanayomilikiwa na Korea Kaskazini
Spread the love

KOREA Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi, ambalo ni la tatu kurushwa na taifa hilo katika kipindi cha wiki tatu, anaandika Hamisi Mguta.

Kombora hilo aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 (maili 280) kabla ya kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan, hatua iliyoifanya Japan kulalamika vikali.

Wachanganuzi wanasema jaribio hilo ni ishara kwamba Korea Kaskazini inapiga hatua katika kuunda makombora yanayoweza kubeba mabomu.

Korea Kaskazini imeendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa linaloizuia kufanya majaribio yoyote ya makombora au silaha za nyuklia, na imeongeza kasi na idadi ya majaribio hayo katika miezi ya karibuni.

Kikosi cha Jeshi la Marekani Bahari ya Pacific kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.

Waziri kiranja wa Japan Yoshihide Suga amewaambia wanahabari kwamba kombora hilo lilianguka katika eneo la bahari lililo kati ya visiwa vya Sado na Oki nchini Japan, katika eneo la pamoja la kiuchumi la visiwa hivyo viwili.

Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema kombora hilo lilipaa juu hadi kilomita 120 angani, na utathmini unaendelea kubaidi “idadi hasa ya makombora yaliyorushwa,” ishara kwamba huenda nchi hiyo ilirusha zaidi ya kombora moja.

Jaribio hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo lilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.

Korea Kaskazini ina hazina kubwa ya makombora ya masafa mafupi aina ya Scud ambayo yaliundwa na Muungano wa Usovieti.

Makombora ya kisasa ya Scud yanaweza kufika umbali wa kilomita 1,000.

Majaribio mawili ya majuzi yaliyofanywa na Korea Kaskazini, ambayo ilisema yote yalifanikiwa, yalikuwa ya makombora ya masafa ya wastani na masafa marefu.

Korea Kaskazini ilisema jaribio la kwanza lilikuwa la kombora jipya lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia.

Pyongyang imekuwa ikifanyia majaribio makombora kwa kasi sana, na wataalamu wanasema huenda inakaribia kufanikiwa kumiliki kombora la masafa marefu linaloweza kufikia maeneo ya Marekani bara.

Korea Kaskazini imekuwa ikisema mpango wake wa kustawisha silaha unanuiwa kukabili hatari kutoka kwa uchokozi wa Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!