Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Kongwa, Chalinze wakumbushwa cha kufanya mradi wa usomaji vitabu
Elimu

Kongwa, Chalinze wakumbushwa cha kufanya mradi wa usomaji vitabu

Spread the love

IDARA  ya Elimu Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma na Wilaya ya Chalinze, Pwani wametakiwa kuhakikisha wanaendeleza mambo muhimu waliyonufaika na Mradi wa Usomaji wa vitabu vya watoto Children Books Program kwa ufadhili na Shirika la Kimataifa Pestalozzi Children Foundation (PCF). Anaripoti Danson Kaijage, Kongwa … (endelea).

Maagizo hayo yametolewa na Mkurugenzi wa Elimu shule za msingi Kutoka Tamisemi Dk.George Kidavya aliyemwakilisha Waziri Tamisemi, Sulemain Jafo Katika Halfla fupi ya kukabidhi mradi katika Wilaya hizo mbili iliyifanyika Wilayani Kongwa.

Hafla Hiyo ilitanguliwa na matembezi katika  Shule ya msingi Mkwala ambayo ni Kati ya shule 45 zilizokuwa kwenye mradi wa CBP wilayani Kongwa na kupata maelezo ya Baadhi ya Faida kutoka kwa Mwalimu Sifrasi nyakupola zilizotokana na kuwepo kwa Mradi huo Uliodumu kwa Takribani Miaka tisa katika wilaya hizo.

Nyakupola alisema miongoni kwa faida walizopata ni pamoja na kuongeza ari ya kusoma kwa watoto, kuyaweka madarasa katika mfumo wa kuzungumza kupitia zana za kufundishia watoto, kujenga utamaduni wa kujisomea, watoto kupunguza utoro mashuleni na kuwafanya kuwa watulivu kipindi wawapo madarasani.

Dk. Katherine Fulgence kutoka Chuo cha DUCE, alielezea tathmini ya malengo mahususi ya mradi huo ni kuwafanya watoto katika halmashauri hizo mbili kuongeza umahiri wa kusoma kuchapisha na kusambaza vitabu vya kujisomea mashuleni, kutoka mafunzo kazini kwa walimu wanaofundisha kusoma na kuandika na mafunzo ya haki za mtoto pamoja na kuhamasisha na kuchochea uchapishaji wa vitabu vya watoto kitaaluma.

Hadi kufikia kukabidhi mradi huo, amesema kiwango cha taaluma kabla ya mradi katika shule zilizonufaika na CBP, darasa la IV  hadi la VII kiwango cha ufaulu Kongwa kilikuwa ni asilimia 36 na Chalinze kilikuwa ni asilimia 56.

Hivi sasa Kongwa Darasa la IV ni asilimia  72 na la VII ni asilimia 99 na Chalinze Darasa la IV ni asilimia 100  na la VII ni asilimia 95.

Pia amesema endapo mradi huo utapata ufadhili utawekeza zaidi katika somo la hesabu kwani kwa kipindi chote cha mradi hawakufanikiwa kulifanya somo hilo kwa watoto  kuwa mahiri kutokana na kukosekana kwa machapisho ya vitabu vya somo hilo.

Mwanzilishi wa mradi huo, Mama Beatrice Nalingigwa, alielezea shughuli zilizotekelezwa na mradi huo ni pamoja na walimu walipata mafunzo kazini, hadi kufikia 2019 walimu 559 walipatiwa vyeti na CBP vya ufundishaji bora kati ya walimu 1,125 waliopatiwa mafunzo, vitabu aina 65 vilichapishwa na mradi na kusambazwa nakala 252,000 ambapo kila shule ilipata wastani wa  nakala 5600 na viliwekwa katika maktaba ya shule.

Pia CBP kwa ufadhili wa PCF ulifanikiwa kukarabati madarasa 16 na 0fisi tatu, madawati 300, viti 60 na makabati 12, meza za walimu 40 na shubaka 12 kwa shule tano za halmashauri ya Chalinze ambazo ni Pingo, Chamakweza, Mbala, Vigwaza na Kidogozero.

PCB wameiomba Serikali kuhakikisha inatatua changamoto ya uchache wa walimu, pamoja na ujenzi wa madarasa kwani imekuwa ni changamoto katika utekelezaji mradi huo kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kwa mwalimu mmoja kwani kwa wilaya ya Kongwa kwa wastani katika madarasa ya chini ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 98 na kwa Chalinze ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 52.

Hivyo mradi huo umeleta mapinduzi makubwa kielimu, kifikra, kihisia na kimazingira katika uboreshaji wa elimu kupitia Sera ya Elimu ya Taifa ya Mwaka 2014 katika wilaya hizo mbili na kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule zote zilizokuwa kwenye Mradi.

Alisitiza kuwa mahitaji ya mradi huo kwa sasa ni makubwa kuliko ilivyokuwa mwanzo hivyo Serikali na wadau wengine wanaombwa kuendelea kusapoti mradi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!