January 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Yanga:Matokeo yametuachia kitu cha kujutia

Spread the love

BAADA ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba kocha wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa matokeo haya yamewaachia kitu cha kujutia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea),

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulipigwa leo majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam

Kocha huyo amesema kuwa kwenye mchezo wa leo walipaswa kupata matokeo lakini wachezaji wake walipunguza umakini na kuruhusu bao dakika za mwisho.

“Matokeo haya yanatuachia kitu kidogo cha kujutia kwa sababu hatukuweza kuondoka kwa alama tatu,” alisema kocha huyo.

Kocha huyo pia ameongezea kuwa kuumia kwa beki wake Lamine Moro kulifanya wachezaji wake kupunguza hali ya kujiamini kwenye mchezo huo.

Cedric Kaze, Kocha wa Yanga

“Wakati Lamine Moro ametoka kulisababisha wachezaji kutojiamini, hata Simba walivyokuwa wanacheza tulipaswa kumiliki mchezo,” aliongezea kocha huyo.

Kaze aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonesha mchezo mzuri licha ya kukili kuzidiwa na Simba katika kipindi cha pili.

Bao la Yanga kwenye mchezo wa leo lilifungwa kwa njia ya mkwaju wa penati dakika ya 31 na Michael Sarpong na baadae katika kipindi cha pili dakika ya 86′ Simba walisawazisha bao hili lililofungwa na Josh Onyango.

error: Content is protected !!