January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Yanga atimkia Mamelodi Sundowns

Riedoh Berdien

Spread the love

KLABU ya Mamelodi Sundowns inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini inatarajia kumtambulisha Riedoh Berdien aliyekuwa kocha wa viungo wa Yanga kujiunga na timu hiyo baada ya kukamilisha mazungumzo nae. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Berdien ambaye alidumu ndani ya Yanga kwa miezi saba tu kabla uongozi kuamua kuachana naye, anatarajia kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Afrika Kusini ambapo atakwenda kuchukua nafasi ya Kabelo Rangoaga aliyetimkia klabu ya Al Ahly ya nchini Misri sambamba na aliyekuwa kocha mkuu wao Pitso Mosimane.

Taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa Berdien anatarajiwa kutambulishwa na mabingwa hao wiki hii mara baada ya kufikiana makubaliano naye wakati wa mapumziko ya michezo ya kimataifa iliyokuwa kwenye kalenda ya Fifa na Caf.

Kwa sasa kikosi cha Memelodi kinanolewa chini ya Manqoba Mngqithi aliyekuja kuchukua mikoba ya Pitso Mosimane mara baada ya kutimkia kwa miamba ya soka nchini  Misri, klabu ya Al Ahly sambamba na baadhi ya makocha aliyekuwa nao kwenye benchi la ufundi.

Riedoh Berdien akiwa kazini na timu ya Yanga

Licha ya kuitumikia klabu ya Yanga lakini pia Birdien alishawahi kuwa kocha msaidizi wa timu za Taifa za wanawake ya Afrika Kusini, ‘Banyana Banyana’ na timu ya Taifa ya Gambia, pamoja na klabu za Free State Star na Chippa United.

Birdien alitua nchini kujiunga na Yanga, Januari, 2020 wakati wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara sawa na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Luc Eymael aliyetimuliwa mara baada ya msimu kumalizika.

error: Content is protected !!