Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Michezo Kocha wa Simba afichua siri ya ushindi dhidi ya Yanga
MichezoTangulizi

Kocha wa Simba afichua siri ya ushindi dhidi ya Yanga

Spread the love

BAADA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amedai kuwa klabu yake ilistahili kushinda mchezo huo wa watani wa jadi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliohudhuriwa na maelfu ya wapenda soko jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, Aussems amesema, “tulistahili kushinda. Tulitengeneza nafasi nyingi sana. Tunamshukuru Mungu tumeshinda.”

Amesema, licha ya kucheza mechi ngumu hivi karibuni, wachezaji wake walijitahidi kucheza vizuri na kuwapongeza kwa kile walichokifanya.

“Leo niwe mkweli baada ya dakika ya 60 hadi 65 tulivyogongesha mwamba na kutengeneza nafasi nyingi nilishaanza kufikili kama yale yale yaliotokea katika mchezo uliopita. Lakini nashukuru kuwa baadae tulifanikiwa kupata bao,” alieleza.

Aussems amesema, “nafikili tulistahili kushinda na nawapongeza wachezaji wangu kwa kuwa walicheza mechi ngumu siku nne zilizopita na kwamba nina furaha ya ushindi na najivunia kuwa nao.”

Goli pekee la Simba katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji wao Meddy Kagere, katika dakika 71 ya mchezo kwa njia ya kichwa.

Jikumbushe sehemu ya mchezo huo kwa kufuatilia  video kamili hapa chini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

error: Content is protected !!