May 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba: Tumekuja kushinda fainali

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck

Spread the love

KULEKEA mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Namungo FC, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Sven Vandenbroeck amesema, wamekwenda Sumbawanga Mkoa wa Rukwa kucheza fainali hiyo ili kushinda ubingwa na si vinginevyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… endelea

Mchezo huo unachezwa kesho Jumapili tarehe 2 Agosti 2020 kwenye Uwanja wa Nelson Mandela uliopo mkoani humo ambapo Simba watakuwa wanasaka taji la tatu kwa msimu huu.

Akizungumza mapema leo Jumamosi na waandishi wa habari, Kocha huyo amesema, wanakila sababu kushinda mchezo huo wa kesho na kuahidi, kutumia wachezaji wake bora ili aweze kupata matokeo.

“Ni mchezo ambao tunahitaji kushinda hivyo tutatumia wachezaji wetu wote bora ili kuhakikisha tunashinda. Wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo,” amesema mkocha huyo

Kwa upande wa Nahodha wa kikosi hicho, John Bocco amesema, wamejiandaa vizuri na wanakutana na mpianzani ambaye wanamjua hivyo wanacho hitaji wao ni kutengeneza historia kwa kuchukua mataji matatu msimu huu.

“Tunaamini tunakutana na mpinzani mzuri, anatujua na sisi tunamjua lakini tunaamini maandalizi yetu na kwa kumtanguliza Mungu tunaamini kesho tunaenda kupambana na kushinda ubingwa wa FA.”

“Tunachoangalia sana kesho ni kuandika historia kuchukua makombe matatu msimu huu (Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na kombe la FA). Ni moja ya malengo tangu tunaanza msimu na hiyo ni kama hamasa kwetu ya kutafuta ushindi hapo kesho,” amesema Nahodha huyo.

Simba imefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe hilo baada ya kuifunga Yanga kwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa nusu fainali, huku Namungo FC ikiiondoa Sahare All Star kwa kupata ushindi wa bao 1-0.

error: Content is protected !!