Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Klopp amwaga chozi, ubingwa wa Liverpool
Michezo

Klopp amwaga chozi, ubingwa wa Liverpool

Jurgen Klopp
Spread the love

KOCHA wa timu Liverpool Jurgen Klopp ameonesha hisia kali za furaha mara baada ya timu yake kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu nchini England, baada ya Manchester City kufungwa na Chelsea kwa mabao 2-1. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Klopp ameonesha hisia hizo wakati akifanya mahojiano na kituo cha Sky Sport mara baada ya mchezo kati ya Chelsea na Manchester City kumalizika na kusema kuwa hakuwa na wazo kama atajisikia hivi.

“Tulilazimika kuwashawishi watu na hivi ndivyo tulivyofanya kwa pamoja, ni wakati mzuri, nimezidiwa kabisa sikujua ningejisikia hivi,” alisema Klopp.

Toka mara ya mwisho kuchukua ubingwa Jurgen Klopp anakuwa kocha wa tisa kukinoa kikosi hicho na kufanikiwa kumaliza ukata wa taji la Ligi Kuu.

Makocha hao waliopita tangu mwaka 1990 ni Graeme Souness (1991–1994), Roy Evans (1994-1998), Gerard Houllier (1998-2004), Rafael Benitez (2004-2010), Roy Hodgson (2010-2011), Kenny Dalglish (2011-2012), Brendan Rodgers (2012-2015) na Jurgen Klopp (2015-2020)

Liverpool iliwalazimu kusubili kwa muda wa miaka 30 kutwaa taji la Ligi Kuu nchini England toka walivyofanya mara ya mwisho 1990, chini ya kocha Kenny Danglish.

Ubingwa huu utakuwa wa 19, kwa klabu hiyo wakiwa nyuma ya Manchester United wenye mataji 20.

Baada ya taji hilo, Liverpool imeweka rekodi ya kutangaza ubingwa ikiwa imesalia michezo saba na kuvunja rekodi iliyowekwa na Manchester United walioiweka kwenye msimu wa 2000/01 walitangaza ubingwa wakiwa wamesalia na mechi tano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!