Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kitengo cha kusaka masoko ya nje ya mazao chaanzishwa
Habari Mchanganyiko

Kitengo cha kusaka masoko ya nje ya mazao chaanzishwa

Spread the love

SERIKALI imeanzisha kitengo maalum cha kitakachowezesha kupatikana kwa masoko sahihi ndani na nje ya nchi ili kuwafanya wakulima kutozalisha kwa mazoea bali kwa faida. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba amesema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakilima mazao kwa mazoea tena baada ya kuona wakulima wenzao wameuza sana na kupata faida mwaka uliopita bila kukumbuka kama huenda masoko ya zao hilo hayawezi kuwepo kwa mwaka unaofuata.

Mgumba amesema, kitengo hicho chenye utaratibu wa kutafuta masoko sahihi na kuweka taarifa sahihi kwa ajili ya wakulima kina uwezo wa kusaidia wakulima kupiga hatua ya kilimo na kuona tija ya kilimo kwa maendeleo.

“Kurudia mazao ya kilimo ya msimu uliopita eti sababu mkulima mwenzako aliuza akapata faida kunaweza kusababisha mkulima kila mwaka kupishana na hela baada ya kukosa soko,” amesema Mgumba.

Aidha Mgumba ametolea mfano zao la ufuta ambalo mwaka jana 2017 wakulima waliuza Sh. 3,000 kwa kilo na kuona faida ya kilimo ambapo bila kufuata utaratibu na maelekezo wakulima wanaweza kuanza kuzalisha ufuta kwa wingi mwaka huu kwa lengo la kupata faida.

Amesema, kitengo hicho kitawasadia wakulima kupata masoko kufuatia kuwa soko ndio moyo wa biashara ikiwa wakulima watakuwa na nia ya kufanya kilimo biashara.

“Mkulima ni lazima ajue analima kiasi gani anamuuzia nani ili wakulima wasiweze kupata hasara, kama ilivyo kwenye zao la Tumbaku, mtu ukimuona analima Tumbaku jua anajua pa kuuza na bei yake, na Serikali inataka kilimo kwa sasa kiwe na mfumo huu kwa manufaa ya wakulima nchini,” amesema.

Hata hivyo amewaasa maofisa kilimo na ugani nchini kuwa karibu na wakulima ili waweze kwenda sambamba na malengo ya Serikali ya kuinua Kilimo nchini.

Mmoja wa wakulima wa zao la mbogamboga wilayani Mvomero mkoani hapa Agnes Rodgers ameishukuru Serikali kwa mpango waliouanzisha huku akiomba Serikali kuendelea kuboresha suala la Kilimo hapa nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!