Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kisukari, Saratani yapunguziwe mzigo wa matibabu
Habari za Siasa

Kisukari, Saratani yapunguziwe mzigo wa matibabu

Hospitali ya magonjwa ya Kansa ya Ocean Road
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum (CUF), Rukia Ahmed ameitaka serikali kuwaondolewa ukali wa gharama za matibabu, waathirika wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza hasa kisukari na saratani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Rukia ametoa wito huo wakati akiuliza swali kwa Wizara ya Afya, akisema kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwemo kisukari na saratani matibabu yake yamekuwa ghali na hayako ya moja kwa moja, na kuitaka serikali kutoa msimamo wake katika kuboresha huduma ya waathirika wa magonjwa haya hususan kwenye matibabu.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya, Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla amesema serikali inaendelea kuhimiza wananchi hasa waathirika wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kujiunga na bima ya afya ili kupunguza mzigo wa gharama za matibabu.

“Gharama za magonjwa yasiyo ya kuambikiza ni kubwa mno, serikali imeanzisha mkakati wa kuhamasisha watu kuishi maisha ya afya, kuangalia vyakula wanavyokula, kufanya mazoezi, hivyo ili kuepuka gharama za kutibu . Tunaendelea kuhamasisha zaidi kinga kuliko tiba, kuna mkakati watu wote wawe na bima ya afya ili huo mzigo wa gharama usiweze kuwa mkubwa na badala yake ubebwe na jamii,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!