SOULEYMAN Keita, kiongozi wa kundi la waasi la Ansar Dine la Iyad Ag Ghali nchini Mali na wenzake 18, mwishoni mwa wiki wamehukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya ugaidi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa ……..(endelea).
Mahakama nchini Mali, imewahukumu kifo kwa kukutwa na hatia ya ugaidi ikiwa ni pamoja na kumiliki silaha za kivita pia kushiriki mauaji ya raia wasio na hatia.
Keita na wenzake, wametajwa kushirkiki kwenye shambulio lililotokea katika Mji wa Konna mwaka 2013 na kusababisha mauaji ya watu wengi.
Mahakama nchi ni humo imeeleza, watu hao wanaojiita wana jihadi wanaojinasibisha na Uislam, wamekuwa wakishiriki mashambulizi kadhaa kwenye mji huo ulio Kusini mwa Mali pamoja na nchi za Cameroon na Burkina Faso.
Baada ya shambulizi lililotekelezwa na akina Keita, vikundi vya usalama vya Ufaransa vilivyokuwepo Mali, vililazimika kuingilia kati na kuwatimua wapiganaji hao.
Keita anatajwa kuwa kiongozi hatari anayeendesha operesheni ya kusaka wapiganaji wapya wa kundi la Ansar Dine, na mara kwa mara amekuwa akishiriki mashambulio kwenye mipata ya nchi mbili zinazopakana na Mali.
Keita alikamatwa mwaka 2016 akiwa na wenzake wawili kutoka Burkina Faso, baada ya kufikishwa mahakamani na wenzake, walikiri kufanya mashambulio katika maeneo mbalimbali katika nchi hizo tatu.
Leave a comment