Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM , Humphrey Polepole
Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM , Humphrey Polepole

Kimbisa, Maghembe kuwania ubunge wa Afrika Mashariki

CHAMA Cha Mapinzuzi CCM leo kimeteua wanachama 12 wa Tanzania Bara na Visiwani watakaoomba ridhaa kwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, anaandika Hamisi Mguta.

Majina hayo yametangazwa kupitia kwa Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, katika ofisi  ndogo Lumumba.

Polepole amesema chama hicho kimezingatia suala ya jinsia ambapo kuna idadi sawa ya wagombea wanaume na wagombea wanawake, huku pia suala la maadili likizingatiwa kwa kina.

Kwa Tanzania Bara kimeteua wajumbe nane ambao ni Zainab Rashid Mfaume Kawawa, Happiness Lugiko, Fancy Haji Nkuhi na Happiness Mgalula kwa upande wa wanawake.

Huku upande wa wanaume Dk. Ngwaru Jumanne Maghembe, Adam Omari Kimbisa, Anamringi Issay Macha na Charles Makongoro Nyerere.

Amesema wajumbe hao wote wamewachuja na kubaini kwamba wanazo sifa za kitaaluma hivyo wanachama wa chama hicho wasiwe na wasiwasi.

“Tumeyapitisha kwenye tanuli la kuwatazama uadilifu wao, uchapakazi wao, kwa sababu maadili ni jambo muhimu sana, ” amesema Polepole.

Kwa upande wa Visiwani kimewachagua Maryam Ussi Yahya, Rabia Abdallah Hamad kwa wanawake na wanaume ni Abdallah Hasnu Makame na Mohamed Yussuf Nuh.

CHAMA Cha Mapinzuzi CCM leo kimeteua wanachama 12 wa Tanzania Bara na Visiwani watakaoomba ridhaa kwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, anaandika Hamisi Mguta. Majina hayo yametangazwa kupitia kwa Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, katika ofisi  ndogo Lumumba. Polepole amesema chama hicho kimezingatia suala ya jinsia ambapo kuna idadi sawa ya wagombea wanaume na wagombea wanawake, huku pia suala la maadili likizingatiwa kwa kina. Kwa Tanzania Bara kimeteua wajumbe nane ambao ni Zainab Rashid Mfaume Kawawa, Happiness Lugiko, Fancy Haji Nkuhi na Happiness Mgalula kwa upande…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Hamisi Mguta

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube