Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kilio uvunjwaji msikiti UDOM chafikishwa JPM
Habari za Siasa

Kilio uvunjwaji msikiti UDOM chafikishwa JPM

Spread the love

KILIO kinachotokana na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuamuru kuvunjwa kwa msikiti uliokuwa ukijengwa kwa ajili ya ibada ya waumini wa Dini ya Kiislam, kimefikishwa kwa Rais John Magufuli. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza kwenye kikao cha Rais Magufuli na viongozi wa dini leo tarehe 23 Januari 2019, Sheikh Mussa Kundecha, Amiri Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam amefikisha kilio hicho na kushauri namna njema ya kulimaliza.

“Wiki moja iliyopita tulijiwa na wenzetu Waislamu kutoka Dodoma, wakiongelea suala la msikiti. Tunashukuru serikali kwa kutenga eneo la ibada, ni jambo muhimu,” amesema Sheikh Kundecha.

Amesema kuwa, ni muhimu kuwa na maeneo ya ibada katika maeneo ya kijamii hasa kutokana na utaratibu wa Ibada ya Kiislam na kwamba, kwa kuzingatia hilo uongozi wa chuo awali ulitoa eneo na Waislam walianza kuchangishana kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo.

“Waislam wakawa wanachangishana ili kujenga nyumba hiyo ya ibada lakini ghafla taarifa ya chuo ikatolewa kusitisha ujenzi wa msikiti huo,” amesema Sheikh Kundecha na kuongeza;

“Tuliamini labda taarifa hiyo ya kusitisha ilitolewa ili kuweka baadhi ya mambo sawa lakni mara wakaleta magreda na kuanza kuubomoa na na mnajua pesa za kuchangisha zilivyo ngumu. Sasa leo anasikia greda imevunja, hii inaleta shida kwa wanaochangia. Nakuomba maeneo ya namna hiyo uyatazame ili isilete mizozo.”

Kumekuwepo na taarifa zinazosambaa kuhusu kadhia ya uvunjwaji wa msikiti huo kulikoambataka na kubadilishwa vituo vya kazi kwa watumishi wa Dini ya Kiislam.

Wanaotajwa kuondolewa UDOM na kupelekwa kwenye taasisi zingine ni pamoja na Dk. Mariam Khamisi aliyepelekwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), DK. Yusuph Kambuga (ADEM Bagamoyo), Dk. Masoud (DIT), Dk. Ibuni Kombo, Khamisi Mkanachi (UDSM).

Wengine ni Mohammed Mwandege (Arusha Atomic Energy), Omar Simba (Wizara ya Ardhi), Subira Issa Sawasawa (Wizara mambo ya Ndani), Wema Mbegu (Wizara ya Ardhi), Aziz Gendo (Arusha Technical) na Dk. Mwinyikondo Ameir (UDSM-Mbeya).

Baada ya tukio la uvunjwaji wa msikiti huo, taasisi za kiislam zimekuwa zikitoa matamko kuonesha kutoridhishwa na hatua iliyochukuliwa na uongozi wa chuo hiko.

Hatua ya uvunjwaji wa msikiti huo na kuhamishwa kwa watumishi wa chuo hicho wa Dini ya Kiislam iliyokana na madai ya kuhusika kumloga na kumuua Prof. Edig Beautus Mobofu aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo tarehe 18 Desemba, 2018.

Madai zaidi yanaelezwa kuwa Prof. Edig Beautus Mobofu alilogwa kwa sababu ya kusimamisha ujenzi wa msikiti huo ambapo kutokana na hisia hizo hasi, tarehe 9 Januari , 2019, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo aliyeshika nafasi ya Prof. Mobofu, Prof. Peter Msoffe alitoa amri ya kuvunja msikiti huo kwa madai kuwa, amepokea amri hiyo kutoka juu.

Kwenye kikao hicho Rais Magufuli amewapa nafasi viongozi hao wa kiroho kueleza kile wanachotaka kwa malengo ya kuendeleza Amani na ushirikiano kwa manufaa ya taifa.

Sheikh Kundecha amemwambia Rais Magufuli kwamba, kuna kila sababu ya kuangalia namna ya kuliweka sawa suala hilo kutokana na umuhimu wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!