Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kilichoonekana kwenye video ya Mbowe Kisutu
Habari za SiasaTangulizi

Kilichoonekana kwenye video ya Mbowe Kisutu

Spread the love

VIDEO ya Freeman Mbowe na wenzake, iliyoibua mvutano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hatimaye imeoneshwa leo tarehe 19 Agosti 2019. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kwenye video hiyo, Mbowe anaonekana akiwaambia wafuasi waliokuwa kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi Salum Mwalimu, aliyekuwa mgombea kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni, waende kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kindondoni.

Katika kesi hiyo namba 112/2018, shahidi namba sita – Koplo Charles – wa upande wa Jamhuri ndiye aliyewasilisha ushahidi wa video hiyo, ukilenga kuithibitishia mahakama, kwamba Mbowe na wenzake walifanya uchochezo kwenye shitaka hilo.

Ushahidi huo wa video ulioneshwa mahakamani hapo kwa kutumia Projector, baada ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba kutoa uamuzi katika maombi ya upande wa Jamhuri ya kutaka ushahidi huo kutumiwa mahakamani hapo.

Katika uamuzi wa ombi hilo, Hakimu Simba alitoa dakika 40 kwa ajili ya video hiyo kuoneshwa kwa kutumia vifaa vya nje (external device).

Kwenye zoezi hilo, Koplo Charles alisaidiwa na mtaalamu wa IT, Nazari Moshi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuunganisha kamera yake na vifaa vya nje vya mahakama hiyo kwa ajili ya kuonesha video hiyo aliyoigawa mara mbili (Min div 1 &2).

Koplo Carles alionesha video ya kwanza aliyoipa jina la ‘Mkutano wa Chadema wa mwaka 2018’ ambayo ilionesha baadhi ya  viongozi na wabunge wa Chadema wakiongozwa na  Mbowe, Mwenyekiti Chadema – Taifa na  Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa chama hicho, wakimnadi Mwalimu kwenye uchaguzi huo wa marudio.

Video ya kwanza yenye dakika 56 na sekunde 37, ilionesha wabunge kadhaa wa Chadema akiwemo, John heche (Tarime Mjini), Cecil Mwambe (Ndanda), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) wakitoa hotuba zao za kumnadi Mwalimu.

Baadaye, video hiyo ilimuonesha Mbowe akihutubia wananchi waliohudhuria katika mkutano huo na kisha kumkaribisha Mwalimu kwa ajili ya kunadi sera zake. Video hiyo iliishia hapo

Video ya pili; yenye urefu wa dakika 25 na sekunde 55, iliyomuonesha Mbowe akihutubia kisha kuwataka wananchi kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni.

Baada ya ushahidi huo wa video kumalizika, Hakimu Simba ameiarisha kesi hiyo kwa dakika 30, na kupanga kumalizia usikilizwaji wa shahidi namba sita ambaye ni Koplo Charles katika chumba cha mahakama hiyo namba moja.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online kwa taarifa zaidi kuhusu kesi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!