January 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kilichomtoa uhai Askofu Banzi chatajwa

Spread the love

CHANZO cha kifo cha Antony Banzi, aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga kimetejwa kuwa ni ugonjwa wa koo. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Kwenye iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), imeeleza kwamba Askofu Banzi alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambapo mauti yalimkuta.

Kiongozi huyo wa kiroho kabla ya kufikwa na umauti, alikwenda India kwa ajili ya matibabu na akarejea nchini ingawa alikuwa hajapona vizuri.

Na kwamba, baada ya kupata matibabu awali, aliruhusiwa kurejea nyumbani kwake kutokana na afya yake kuimarika.

Pia askofu huyo alikuwa Mwenyekiti na Mlezi wa Mashirika ya Masista na Watawa wote Tanzania ambapo Septemba mwaka huu, alitimiza miaka 25 ya uaskofu.

error: Content is protected !!