Kikwete aishauri Yanga kumwacha Morrison

Spread the love

RAIS mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewataka mashabiki wa klabu ya Yanga kutoumizwa kichwa na sakata la mchezaji Bernard Morrison kuhamia kwa watani zao Simba akisema kama wao wamemchukua mchezaji huyo na Yanga watafute mwengine wa kumchukua. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… endelea

Maneno hayo ameyatoa jana Jumapili tarehe 30 Agosti 2020  alipokuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha tamasha la ‘Wiki ya Mwananchi’ lilofanyika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watazamaji zaidi ya elfu sitini.

Kikwete alisema, ni kawaida kwa timu za Simba na Yanga kuibiana wachezaji toka miaka ya nyuma kwani ndio maisha ya timu hizo.

Bernard Morrison 

“Hili la kuibiana wachezaji halikuanza na Morrison, limeanza enzi na enzi, kwa hiyo haya wala yasiwasumbue akili, wakichukua Morrison na nyinyi tafuteni wa kumchukua” alisema Kikwete ambaye ni shabiki wa Yanga

Aidha, alisisitiza  Yanga inapaswa kuwekeza kwa vijana pamoja na wachezaji wa ndani ili kuepuka mambo kama hayao na kuwataka mashabiki wa timu hiyo wasiwe wanyonge kwa kuondoka mchezaji huyo badala yake waachane naye.

Morrison tayari ameanza kuitumikia Simba na jana Jumapili, alifunga bao moja katika ushindi wa 2-0 iliyoupata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Pia, Morrison alisababisha bao la kwanza kwa kuangushwa eneo la 12 na mwamuzi kuamri mkwaju wa penati uliokwamishwa wavuni na Nahodha John Bocco.

Tamasha hilo lilihitimishwa kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na klabu ya Aigle Noir kutoka nchini Burundi na mchezo huo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ikumbukwe Morrison aliingia nchini 17 Januari, 2020 akitokea nchini Ghana na kujiunga na Yanga na baadaye kuamua kutimkia Simba baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na Yanga na kuamua kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

RAIS mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewataka mashabiki wa klabu ya Yanga kutoumizwa kichwa na sakata la mchezaji Bernard Morrison kuhamia kwa watani zao Simba akisema kama wao wamemchukua mchezaji huyo na Yanga watafute mwengine wa kumchukua. Anaripoti Kelvin Mwaipungu... endelea Maneno hayo ameyatoa jana Jumapili tarehe 30 Agosti 2020  alipokuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha tamasha la 'Wiki ya Mwananchi' lilofanyika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watazamaji zaidi ya elfu sitini. Kikwete alisema, ni kawaida kwa timu za Simba na Yanga kuibiana wachezaji toka miaka ya nyuma kwani ndio…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!